SIMU ZA KISASA (SMARTPHONES) ZINAVYOWEZA KUTUMIKA KUPIMA NGUVU ZA KUIUME

Watafiti wa Marekani wamegundua kifaa kipya cha ‘smartphone’ kilicho na uwezo wa kupima na kubaini kama mbegu za uzazi za mwanaume zina uwezo wa kumfanya mwanamke kuwa mjamzito.
Kutokuwa na uwezo wa kuzaa kumewaathiri watu zaidi ya milioni 45 duniani. Zaidi ya 40% ya matatizo ya uzazi yanasababishwa na kiwango hafifu cha mbegu za kiume.
Teknolojia iliyochambuliwa katika makala ya ‘Science Translation medicine’ imelenga kuleta urahisi kwa wanaume kujipima wenyewe uwezo wa mbegu zao za uzazi.
“Tumetaka kuleta utatuzi na kufanya upimaji wa uwezo wa mbegu za kiume kuwa rahisi na unaopatikana kama vile vipimo vya ujauzito vya wanawake” alisema Hadi shafee daktari katika kitengo cha uhandisi wa madawa katika hospitali ya Wanawake Brigham.
“Wanaume hutakiwa kuleta manii katika hospitali hali ambayo huwafanya kuwa na woga  na kuudhika”
Kipimo hiki kipya, kinaweza kutoa majibu ya manii ndani ya muda wa dakika 5.
Kipimo hichi kinafanya kazi kupitia muunganiko wa ‘smatphone’ na chombo cha kuwekea manii, ilieleza ripoti hiyo.
Watafiti hao, walikifanyia majaribio kipimo hicho kwa kutumia manii za wanaume 350 katika kituo cha ‘Massachusetts General Hospital fertility Centre’.
Kifaa hicho kilitoa majibu yenye ukweli kwa asilimia 98. Gharama ya kifaa hicho ni dola za kimarekani 4.45 sawa na shilingi za kitanzania 10000 tu.
Waliongeza kuwa uwepo wa kifaa hicho utarahisisha ufuatiliaji wa afya za uzazi kwa watu binafsi pasipokuwa na haja ya kwenda hospitali.
Aidha kifaa hicho bado kipo katika hatua za mwisho za majaribio na kitazinduliwa rasmi kwa matumizi baada ya kukaguliwa na kitengo cha ‘US Food and Drug Administrational Approval’ chenye mamlaka ya kuthibitisha kama kifaa hicho kinafaa kwa matumizi.
– The Citizen
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post