STAMINA APATA LEBO YA KUMSIMAMIA

Msanii wa muziki wa hip hop Stamina amefunguka kwa kusema kuwa tayari amesaini mkataba na label kubwa ya muziki nchini.

Rapa huyo ameiambia Bongo5 kuwa hawezi kujitangaza kwa kuwa siyo jukumu lake.
“Nashukuru Mungu nimesaini na label kubwa sana hapa nchini na tayari hapa ninapozungumza tumeanza kufanya kazi pamoja, hata project ambazo nazifanya kwa sasa zipo chini yao. Lakini kwa sasa siwezi kuitaja ni label gani wao ndio wanatakiwa kufanya hivyo,” alisema Stamina.
Aliongeza, “Muziki umebadilika sana sasa hivi, siwezi kufanya kila kitu, lazima uwe na team ambayo itakuwa inafanya kazi zako nyingine, kwahiyo kwangu mimi naweza kusema hii ni safari mpya na Stamina ambayo itakuwa na mambo mengi mazuri,”
Pia rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya wimbo wake mpya ambao amedai atauachia muda wowote.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post