STEVE NYERERE: SIASA ZIMECHANGIA KUUA SOKO LA FILAMU ZA TANZANIA

Mchekeshaji maarufu hapa nchini, Steve Nyerere amesema kuwa wasanii hasa waigizaji kujiingiza katika siasa ni moja ya sababu zilizopelekea kupotea kwa mvuto wa filamu nchini.
Steve amesema hayo ikiwa ni siku chache tokea kufanyika maandamano ya baadhi ya wasanii wa filamu kuishinikiza serikali kuwaondolea kodi katika filamu zao au kuhakikisha inakusanya pia kodi za filamu za nje ambazo zinakuwa zinapakuliwa katika mitandao kitu kinachopelekea kuua soko la ndani la filamu za bongo.
Steve ameongeza kuwa wasanii wenzake kwenda kupambana na wauzaji wadogo wadogo ni dhambi kwani kiini cha matatizo kipo kwao wenyewe,  na hiyo yote imechangiwa na wasanii kuacha kazi zao na kufanya siasa.
Mimi naomba niongee ukweli leo, kilichotuuwa bongo movie ni siasa. Kipindi tupo kwenye uchaguzi mkuu kulikuwa na makundi mawili ya siasa ambayo yalikuwa yanawasapoti wagombea tofauti ndani ya tasnia ya filamu. Lakini cha kushangaza uchaguzi tumeumaliza vizuri ila badala ya kuendelea na kazi zetu za uzalishaji wa filamu bado tunaendeleza kazi za watu ambazo hatuna hata utaalamu nazo“- alisema Steve.
Pamoja na hayo Steve Nyerere ameongeza kuwa wapo wasanii wa filamu ambao wameweza kutenganisha siasa na filamu na kwamba hao ni wale ambao wamebahatika kuvaa kofia hizo mbili ndio maana wametumia busara zao kutotumika kwenye maandano ya watu wachache.
Unajua pamoja na siasa kuna watu pale bongo movie wana kofia mbili mbili mfano mimi niliwahi kugombea Ubunge wa Kinondoni kwa hiyo lazima najua nini nafanya, Irene Uwoya ni Mbunge pale na anayo nafasi yake ndani ya chama  ikitokea bahati mbaya mbunge wa viti maalumu akaanguka yeye ndiye atakayeziba pengo au Wema Sepetu na harakati aliozonazo sasa hivi na ndio maana hata ukiangalia kwenye maandamano watu waliyoyafanya wao walikaa pembeni siyo kwamba siyo wasanii , hapana ni wasanii ambao wamejitambua na hawataki kutumika kwa maslahi ya watu wachache
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post