TAARIFA YA TRA ENDAPO MTU ATAKUTUMIA FEDHA KIMAKOSA KWENYE SIMU

SHARE:

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tahadhari kwa watumiaji wa simu za mkononi kutorudisha pesa kwa mtu aliyetuma kimakosa. T...

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tahadhari kwa watumiaji wa simu za mkononi kutorudisha pesa kwa mtu aliyetuma kimakosa.
Tahadhari hiyo ilitolewa na Mtakwimu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Batholomew Marcel wakati akiwasilisha mada iliyohusu ukuaji wa Sekta ya Mawasiliano na tahadhari za kuzingatiwa na mtumiaji wa Huduma na bidhaa za mawasiliano katika warsha kuhusu Mradi wa Kukuza Utawala Bora na uwajibikaji Tanzania kupitia teknolojia ya dijitali, iliyofanyika Dar es Salaam jana.
“KAMA kuna pesa imetumwa kimakosa kwenye simu yako, hata kama mwenye simu aliyekutumia kimakosa atakuomba na kukubembeleza, usimrudishie yeye, bali ziache na uijulishe kampuni ya simu inayohusika wao ndio wamrudishie” alisema Batholomew.
Aliwatahadharisha watanzania kua makini kwani hali hiyo inaweza kuwasababishia hasara na pengine kuwaingiza katika mikono ya sheria za nchi kama tuhuma za uhalifu mwingine wowote, licha ya kua na nia nzuri ya kurudisha pesa.
Alisema anayepokea pesa iliyotumwa kwake kimakosa anapaswa kuijulisha kampuni husika ya simu vinginevyo anaweza kujikuta anafanya malipo na kutuma pesa kwa wahalifu huku mifumo ikionesha pesa ilikwenda kwake.
Alisema kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT), watu wengi wanatumia simu kutunza, kupokea na kutuma pesa zao hivyo, mikakati bora zaidi haina budi kuwapo ili kuepusha uhalifu wa kimtandao hususani kuhusu pesa mtandao.
“Hapa lazima kuwa makini kwani teknolojia hii ya pesa mtandao pia ina changamoto nyingi na hatari. Kazi ya kurudisha pesa kwa aliyetuma kimakosa, iache ifanywe na kampuni husika ya simu yaani mtoa huduma sio wewe,” alisema.
Changamoto nyingine Marcel alisema ni pamoja na kuibuka wimbi la matapeli wanaojifanya kumfahamu mtu huku wenyewe wakijifanya ni wanasiasa, viongozi wa kikazi, kiserikali, kidini au wanafamilia wanaotoa maelekezo ya kumtaka mtu afanye malipo, kutuma pesa au kuhitaji msaada kwa ulaghai.
Aliwataka watumiaji wa huduma hizo kuwa makini kwani makosa ya kimtandao ni makosa kama yalivyo mengine na yana sheria zake ikiwamo Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015.
Akasema, “Epuka kutunza pesa nyingi katika chombo kimoja kama simu, ukipoteza simu toa kwanza taarifa kwa kampuni husika ya simu ili waifunge kisha sasa, toa taarifa polisi na pia, badili password (namba ya siri) mara kwa mara walau kila baada ya siku 90.”
Akaongeza, “Wengine wanaokumbwa au kulizwa na changamoto za pesa mtandao, ni wale wanaokubali kuaminishwa kuhusu kuwapo biashara inayozaa faida kubwa kwa muda mfupi, kushinda bahati nasibu hata ambazo hawakushiriki na kupata mikopo kirahisi, lakini wakatakiwa kutanguliza malipo,” alisema.
Akasisitiza, “Kuwa makini kwa kuepuka mikopo au dili zinazokutaka kutanguliza fedha…” Kwa upande mwingine, alisema zipo fursa nyingi za mitandao ikiwamo kufanya malipo mbalimbalimbali yakiwamo ya huduma za kijamii kama maji, umeme na ankara nyingine; pamoja na biashara huku wengine wakijiajiri au kuajiriwa katika sekta hiyo ya pesa mtandao.
Katika hatua nyingine, Afisa wa Programu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHCR), Pasience Mlowe, katika warsha hiyo aliiomba Serikali na watunga sera na sheria kuzitazama upya sheria alizosema ni kandamizi ikiwamo Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya Mwaka 2015.
Katika taarifa kuhusu namna Oxfam inavyotumia ICT duniani, Bill Marwa alisema ni pamoja na kuwatumia watu wanaowasaidia na kukusanya pesa toka kwa wafadhili mbalimbali. “Teknolojia hii inatusaidia kuokoa muda na pesa,” alisema.
-Msumba

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: TAARIFA YA TRA ENDAPO MTU ATAKUTUMIA FEDHA KIMAKOSA KWENYE SIMU
TAARIFA YA TRA ENDAPO MTU ATAKUTUMIA FEDHA KIMAKOSA KWENYE SIMU
https://2.bp.blogspot.com/-lf1kqNasbhI/WQOD61KmMqI/AAAAAAAAaPA/yEj7MfAvMoI7Has_jX-OXIKR9RYIv-TdQCLcB/s1600/20130413_blp501.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-lf1kqNasbhI/WQOD61KmMqI/AAAAAAAAaPA/yEj7MfAvMoI7Has_jX-OXIKR9RYIv-TdQCLcB/s72-c/20130413_blp501.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/taarifa-ya-tra-endapo-mtu-atakutumia.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/taarifa-ya-tra-endapo-mtu-atakutumia.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy