TAARIFA YA WIZARA YA ARDHI KUHUSU WATUMISHI WALIOPATIWA MIKOPO YA NYUMBA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi anawakumbusha waajiri wote ambao watumishi wao walipatiwa mikopo ya nyumba inayotolewa na Mfuko wa Mikopo ya Nyumba kwa Watumishi wa Serikali walio na malimbikizo ya madeni ya marejesho hayo, kuwasilisha marejesho ya mikopo iliyotolewa kwa watumishi wao.
Aidha, anawakumbusha pia watumishi waliopewa mikopo kuhakikisha waajiri wao wanawasilisha marejesho ya mikopo hiyo ndani ya siku sitini (60) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Kwa watumishi ambao waajiri wao hawawezi kuwakata mikopo kutoka kwenye mishahara yao kutokana na wao kuwa na madeni ya mikopo mingine, na wengine ambao waliwahi kuwa watumishi wa umma na walikopa kwenye mfuko huu, wanatakiwa kulipa malimbikizo ya madeni yao ndani ya siku sitini (60) kuanzia tarehe ya tangazo hili.
Wizara itaanza kuwachukulia hatua wote watakaokiuka agizo hili kwa mujibu wa sheria na makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wa mkopo.
Waajiri na watumishi wote pia mnakumbushwa kuwa malipo ya mikopo ya nyumba yanalipwa kwa kupitia code 398, kwa akaunti ifuatayo:

Katibu Mkuu – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Jina la Benki:               Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
Jina la Akaunti:           CPS Miscellaneous Deposit EXP Electronic Account
Akaunti Na. 9921169777
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post