TAHADHARI WALIYOICHUKUA WABUNGE WALIOTISHIWA KUTEKWA

SHARE:

Baada ya taarifa ya Mbunge wa Nzega Mjini kwa tiketi ya CCM, hussein Bashe kuwa kuna wabunge 11 ambao wako katika orodha ya watu awnaowez...

Baada ya taarifa ya Mbunge wa Nzega Mjini kwa tiketi ya CCM, hussein Bashe kuwa kuna wabunge 11 ambao wako katika orodha ya watu awnaoweza kutekwa wakati wowote, imesababisha wanaotajwa kurekebisha mienedno yao kuepuka kunaswa huku wengine wakisema kuwa hawana hofu.
Kwa Bashe hali imekuwa tofauti kwa ni amesema kuwa amebadilisha mwenendo wake wa maisha kwa kutoa taarifa kila anakokwenda.
“Nimeanza utaratibu wa kutoa taarifa ya sehemu ninayokwenda. lakini vitisho haviwezi kuubadilisha mfumo wangu a maisha wala kubadilisha ninachokiamini”  alisema Bashe.
Bashe alisema kuwa lailazimika kuliongelea suala hilo bungeni kwani vitisho hivyo siyo dhidi yake pekee bali pia kwa wabunge wengine pamoja na watanzania kwa ujumla.
Mbunge huyo alisema Bungeni kuwa alitekwa na maofisa wa Usalama wa Taifa na kuongeza kuwa kuna wabunge ambao bado wanasakwa na maofisa hao.
Wabunge wanaodhaniwa kuwa ndiyo haswa wanasakwa ni pamoja na Aeshi Hilary- mb. Sumbawanga Mjini(CCM), Mwita waitara -Ukonga(CHADEMA), Tundu Lissu- Singida Mashariki(CHADEMA), Zitto Kabwe- Kigoma mjini(ACT) Mwigulu Nchemba waziri wa mambo ya ndani na Nape Nnauye aliyevuliwa uwaziri na kutishiwa kwa bastola alipotaka kufanya mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Protea.
Vilevile Mbunge Aeshi naye alieleza woga aliokuwa nao na namna alivyoamua kubadilisha mtindo wake wa namna ya kuishi ambapo huwapigia simu watu wake wa karibu kuwaeleza anapokwenda baada ya kudai alitishiwa wazi wazi na kiongozi wa Serikali mkoani Dar es Salaam.
“Mwenzako tangu nitishiwe na yule kiongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, nimekuwa nikiishi kama popo na kila sehemu ninapoenda napiga simu kwa watu mbalimbali kuwaeleza sehemu nilipo. Hata kwenye simu yangu nimetegesha GPS kwa ajili ya wengine kujua eneo nilipo” alisema Aeshi
Mbunge wa jimbo la Ukonga, Waitara alisema kuwa yeye tokea atajwe kwenye orodha ya wanaotakiwa kutekwa amekuwa akiishi kwa hofu kubwa na maisha yake kuwa ya taharuki. Alifika mbali na kusema kuwa eneo wanamoviziwa wabunge hao ili watekwe ni katika geti la kutokea la ukumbi wa Bunge na kuiomba serikalli kulitazama suala hilo kwa umakini zaidi badala ya kulipuuzia tu.
“Maisha yang ni ya wasiwasi kwa sababu mtoa taarifa anasema hao watu wanaotaka kutukamata wapo. Wameelekezwa waje Dodoma na sehemu wanayotuvizia ni kwenye geti la kutokea bungeni.” alisema waitara
“Nimechukua hatua za ulinzi binafsi kwa namna ambayo siwezi kusema ni ulinzi upi, ila kwa sasa nimekuwa mwangalifu na sehemu ninazokwenda kutembea” aliongeza.
Kwa upande wa wabunge wengine hawakuonesha kutishika na suala hilo la utekwaji nyara lililoletwa bungeni na Bashe na kueleza kuwa hakuna kitu kama hicho na watu wapuuzie kwani i propaganda zinazolenga kuichafua nchi na kuwapa hofu wananchi wake.
Moja ya wabunge waliotajwa katika orodha na hawajaonyesha kushtushwa ni Zitto Kabwe ambaye alisema kuwa hiyo ni hali ya kupeana hofu ambayo ni lazima ipuuzwe kwani inaweza kuacha taharuki kwa wananchi.
“Nadhani ni mambo ya kupeana hofu tu. Kwanza, sijafanya lolote la kusababisha nitekwe, niteswe ama kupotezwa. Hivyo habari hizi nazidharau kwa sababu sioni sababu kwanini nitekwe” alisema Zitto
Zitto aliwasilisha hoja bungeni ya kutaka iundwe kamati teule ya kuchunguza matukio yote ya utekaji na wananchi kuteswa. Alisema kama kweli kuna watu wenye mpango wa kumteka, wajipange vizuri na wajiandae sana.
“Wanaweza kupanga kuniteka wakanitafuta wakakuta mti wa mrumba au bwawa la Karosho au ziwa Tanganyika. Wathubutu tu wataona” alisema Zitto
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba, ambaye pia alitajwa kama moja ya wabunge ambao wanaweza kutekwa muda wowote, yeye alieleza kuwa hana hofu yoyote ya kutekwa na anapenda kuwaambia wabunge wengine waliopata tishio la kutekwa wasiwe na hofu kwa kuwa jambo hilo halipo.
“Ngoja nikuambie, kwanza hakuna kitu kama hicho. Pili hakuna sababu ka,a hiyo na tatu nchi yetu haijafikia hatua kama hiyo. Nadhani ama hofu ya watu au watu wenye nia ya kutengeneza taharuki na kutaka kuchafua nchi yetu. Kwa maana hiyo mimi kama Waziri ninayeshughulikia masuala ya usalama wa raia kwa ujumla ninawaambia hakuna kitu kama hicho.” alisema Mwigulu
HT: Mwananchi

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: TAHADHARI WALIYOICHUKUA WABUNGE WALIOTISHIWA KUTEKWA
TAHADHARI WALIYOICHUKUA WABUNGE WALIOTISHIWA KUTEKWA
https://4.bp.blogspot.com/-qb4iYyrkk7A/WPJvWQ24wMI/AAAAAAAAZjk/nUnrli97-XQwJ5EZKUeXom5VPbyLLyUhACLcB/s1600/NNN.webp
https://4.bp.blogspot.com/-qb4iYyrkk7A/WPJvWQ24wMI/AAAAAAAAZjk/nUnrli97-XQwJ5EZKUeXom5VPbyLLyUhACLcB/s72-c/NNN.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/tahadhari-waliyoichukua-wabunge.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/tahadhari-waliyoichukua-wabunge.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy