TAJIRI ALIYEOA WAKE WAWILI KWA ‘MPIGO’ DAR ASIMULIA MAISHA YAKE YA NDOA

Javan Bidogo, ambaye ni mfanya biashara mkubwa  hapa nchini amefanya tukio la aina yake ambalo limezua taharuki kwa watu wengi.
Bidogo mwenye umri wa miaka 42, ameamua kufunga ndoa na wanawake wawili kwa wakati mmoja tofauti na ilivyozoeleka kwamba ndoa za mitara huwa mke wa pili anaolewa baada ya mume kuishi kwa muda na mke wa kwanza.
Pichani: Bidogo akiwa na mke wake Asha Juma siku ya harusi yao.
bbb
Tukio hili limewaacha wengi wakiwa vinywa wazi na wengine kushindwa kutambua ni nini sababu iliyompelekea Bwana Bidogo kufanya uamuzi huo.
Pichani: Bidogo katika sherehe ya harusi na mkewe Elvas Kulengwa.
b2
Kwa upande wake Bidogo, alieleza kuwa amefanya hivyo kwa kuwa aliwapenda wake zake wote wawili na hakuwa tayari kumuacha hata mmoja.
“Nimedumu katika uchumba na wanawake hawa kwa miaka miwili na nusu kabla sijawaoa. Sikutaka kuwaosa wote ndiyo maana nikafanya maamuzi. Nilizungumza na Asha  (34) akakubali na pia Elvas (21) naye akabariki hilo. Na kwa kuwa walikuwa wachumba zangu wa muda mrefu, niliona ni sahihi na nina haki kisheria” alisema Bidogo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam Jumatatu akitoke dubai kwenye fungate.
Hata hivyo wake zake, Elvas Kulengwa na Asha Juma wanaonekana si tu kukubaliana na suala hilo, bali pia kuifurahia ndoa hiyo ya mitara.
Katika picha zao za harusi zilizofungwa siku mbili tofauti na zile za kabla ya harusi, wanawake hao wameonekana ni wenye tabasamu na furaha wakati wote.
Wakati wa harusi ya mke mkuwa (aliyeolewa wa kwanza), mke mdogo alihudhuria na vivyo hivo kwa mke mdogo pia.
“Niliishi na Asha kwa miaka saba kabla ya kumuoa, na Elvas nimekuwa katika mahusiano nae kwa miaka miwili na nusu. Nilikuwa naishi na Asha lakini baada ya kumpata Elvas niliamua kuishi nao wote.” alisema Bidogo ambaye kitaaluma ni mtaalamu wa miamba.
“Nilimweleza Asha kusudio langu. Alipokubali nilimweleza elvas ambaye pia hakuwa na pingamizi” alisema.
Bwana Bidogo alipoulizwa kuhusu sehemu watakazoishi wake zake alisema kuwa hana wazo la kuwaweka katika nyumba tofauti na haoni kama maisha mapya yatakuwa tatizo.
“Sidhani kama kutakuwa na mabadiliko. Ni watu ambao tunapendana na tunaishi vizuri kwa kweli. Jamii inaweza kuona ajabu lakini nimewapenda ndiyo maana nikaona niwaoe wote wawili.” alisema.
Aliongeza kuwa kabla ya kuchukua uamuzi huo aliishirikisha familia yake na jamii ikamuunga mkono ndipo akaanza taratibu za posa ambapo alipeleka posa kwa Asha na baadaye kwa elvas.
Ndoa hizo zilifungwa na ofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni na sherehe zilfanyika kwa kufuatana kulingana na siku za harusi.”Sikuona kama ni gharama kubwa kufunga ndoa mbili kwa wakati mmoja kwa sababu kamati ya maandalizi ilifanya kazi yake ipasavyo na familia yetu ilitoa mchango mkubwa” alisema Bwana bidogo ambaye ni mfanya biashara wa kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya Javan group of Companies limited.
Alisema kuwa ingawa jamii inaonekana kupigwa na butwaa kwa yeye kuoa wake wawili kwa pamoja, watu wanaomzunguka hasa ndugu na jamaa, wameupenda uamuzi wake.
Wake zake hao hawakutaka kuzungumzia chochote kuhusu ndoa ya mume wao mmoja.
Ndugu wa mmoja wa wake walioolewa, Mgema Kulengwa alisema familia yao inashangazwa na maamuzi ya binti yao kukubali kuolewa na mume mwenye mke mwingine.
“Elvas Hakuweka bayana aina ya ndoa anayofunga, na wanafamilia tulishangaa hasa aliposema anafunga ndoa ya kiserikali.” alisema Mgema”Wazazi na familia kwa ujumla wamelipokea kwa mshtuko kwani siku moja baada ya ndoa tulipigiwa simu kwamba bwana harusi ameoa tena. Baada ya kuchunguza kwa makini tukagundua kwamba hata Elvas anajua fika na alihudhuria. Tumeshtushwa na hili kwa kweli” aliongeza Mgema.
Alisema wakati familia yao inaangalia uwezekano wa kumwita bibi harusi ili wazungumzie utata wa ndoa hiyo, walishangazwa kusikia ana safari.
“Jumatatu alimpigia mzee kumweleza kwamba yupo uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kuelekea Dubai kwa ajili ya fungate. Tukashtushwa tena na picha zilizosambaa mtandaoni akiwa na mke mwenzie na mumewe pamoja”
Baadhi ya wafanyakazi wa Bidogo walisema kuwa amekuwa akionekana na wanawake hao kwa muda sana na hivyo ilikuwa ni wakati mzuri wa yeye kuoa.
Picha tofauti tofauti za Bidogo akiwa na wake zake katika nyakati tofauti 

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post