TANZANIA YASHIKA NAMBA MOJA KWA KUPOKEA NDEGE ZA KIMATAIFA AFRIKA

Tanzania imechangia asilimia 19.3 ya jumla ya wageni wa  kimataifa  waliofika Afrika ikilinganishwa na Kenya iliyochangia asilimia 18.2, Misri asilimia 17.2 na Afrika Kusini  asilimia 12.1 kwa kipindi cha September 2016 hadi Januari 2017.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya kampuni ya ufuatiliaji wa safari za anga ya FowardKeys inayolinganisha data za safari za ndege kutoka shughuli zaidi ya milioni 16 kwa siku na msimamo wa Afrika katika ramani ya utalii duniani.
Ethiopia imeporomoka kwa  asilimia 4.0 kutokana na kupungua kwa wageni kutoka ndani ya mataifa ya Afrika. Kiwango cha watalii kutoka Ulaya na Mashariki ya Kati kimeshuka nchini humo , ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Kikanda, wageni waliofika katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) waliongezeka kwa asilimia 16.4 ingawa Ripoti inaeleza utoaji duni wa huduma ya kuunganisha safari ndefu kama changamoto katika eneo hilo. Kigali ilikuwa ni mji mkuu pekee kikanda kurekodi ukuaji kwa kiwango cha tarakimu mbili na kuwa na uwezo wa safari ndefu kimataifa na zile za ndani ya Afrika.
Kwa ujumla, kuna ongezeko la kiwango cha wageni wa kimataifa wanaofika Afrika kwa asilimia  10.3.
Estelle Verdier, Mkurugenzi wa tovuti ya Jumia Travel inayojihusisha na ‘bookings’ za hoteli ambayo pia hivi karibuni ilianzisha huduma ya kuuzia tiketi za ndege alisema ripoti ya ForwardKeys huonyesha ongezeko la ukuaji wa safari za anga barani Afrika ambayo ni sambamba na ukuaji wa utalii.
Msamaha wa Viza Moroko, kuangaliwa upya vikwazo kutoka Afrika Kusini; na ndege za moja kwa moja kwenda Kenya yalikuwa ni baadhi ya mambo kadhaa yaliyochangia ongezeko la wageni kutoka Asia  kwa asilimia 21.7 kimataifa.
ForwardKeys inaonyesha asilimia 17.3  ya ukuaji wa ‘bookings’ za kimataifa barani kwa nusu ya kwanza ya 2017 na kipindi hichi cha Pasaka ipo katika nafasi ya kurekodi asilimia 53.1 ya ongezeko la jumla ya wageni waliofika ikifuatiwa na ongezeko la asilimia  26.4 mwezi Juni.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post