TANZIA: MWANDISHI WA HABARI JOSEPHAT ISANGO AMEFARIKI DUNIA ASUBUHI YA LEO

Tasnia ya Habari nchini imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na Mwandishi wa Habari Bwana Josephat Isango ambaye amefariki Dunia asubuhi ya leo majira ya saa moja na na dakika 10, wakati akiwa amelazwa Hospitali ya Mt. Maria, Malkia wa Ulimwengu Puma iliyopo Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida.

Awali akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu wa Zote kali Blog, Mdogo wa Marehemu amethibitisha hilo na kueleza kuwa kwa sasa msiba upo kijijini kwao Kisasidi huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.


“Ni kweli Josephat Isango amefariki asubuhi ya leo majira ya saa moja. Alikuwa hapa anapatiwa matibabu akiwa anasumbuliwa na matatizo ya moyo. Taratibu zingine zinaendelea nyumbani huko Kijijini KIsasidi” alieleza Mdogo huyo wa Marehemu.


Hata hivyo alieleza kuwa, wamepanga kufanya maziko siku ya Aprili 18 ambayo itakuwa Jumanne majira ya saa nne asubuhi huko huko Kijijini kwao Kisasida, Barabara ya Arusha.


Marehemu Isango ni miongoni mwa wanahabari mahili na weledi mkubwa katika tasnia ya Habari huku akiwa amepitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. Miongoni mwa vyombo alivyofanyia kazi ni pamoja na kampuni ya Free Media Limited wachapishao magazeti ya Tanzania Daima, Pia aliwahi kuwa mwandishi wa habari wa kampuni ya Halihalisi Publishers inayochapisha magazeti ya Mwanahalisi, Mawio na Mwanahalisi On line na baadae alikuwa Jamii Media.
Marehemu Isango amefariki akiwa na umri wa miaka 44, huku akiwa ni mtoto wa 5 wa familia ya Mzee Isango.


Marehemu mbali na kuwa na taaluma ya Habari, pia mwaka 2010 aliwahi ku kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Singida mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku akichuana vikali na mgombea mwenzake wa wakati huo Mohammed Dewji ‘MO’’.


Mtandao huu wa Zote kali Blog, unatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wanatasnia ya habari popote pale walipo, Ameni.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post