TAZAMA VIDEO YA WIMBO WA NAY WA MITEGO- WAPO (OFFICIAL MUSIC VIDEO)

Mwanamuziki Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la WAPO.
Baada ya Nay wa Mitego kutoa wimbo huo alipitia katika changamoto kadhaa kufuatia kile kilichodaiwa kuwa wimbo huo haukuwa na maadili na hivyo Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuufungia na yeye mwenyewe kukamatwa na Polisi akiwa Morogoro na kusafirishwa hadi Dar es Salaam.
Siku moja baada ya hayo yote kutokea, Rais Dkt Magufuli aliagiza wimbo huo ufunguliwe na msanii aachiwe huru kwani yeye binafsi ameupenda wimbo huo, huku akimshauri Nay auboreshe na kutaja watu wengine kama wakwepa kodi, watumiaji wa dawa za kulevya, wala rushwa kuwa nao WAPO.
Tazama video ya WAPO hapa chini.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post