TOTTENHAM YAIFUNGA BURNLEY NA KUISOGELEA CHELSEA

Tottenham imepunguza pengo na vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea na kuwa pointi saba baada ya baada ya kuifunga timu ngumu ya Burnley kwa magoli 2-0 katika dimba la Turf Moor.

Wageni Tottenham walihaha kusaka goli na hatimaye jitihada zao zilizaa matunda baada ya kupata goli kupitia kwa Eric Dier baada ya wenyeji kushindwa kuizuia krosi ya Christian Eriksen.

Vincent Janssen, alijikuta akiingia katika orodha ya majeruhi watatu wa Tottenham baada ya kuumia akicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu na nafasi yake kuchukuliwa na Son Heung-min ambaye alifunga goli la pili.
                                                             Eric Dier akifunga goli la kwanza la Tottenham
                                                       Son Heung-min akifunga goli la pili la Tottenham 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post