TOTTENHAM YAZIDI KUKOMAA KUIFUKUZIA CHELSEA

Timu ya Tottenham imeendelea kuweka shinikizo kwa vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea kwa kupata ushindi mzuri wa magoli 4-0 dhidi ya Watford.

Katika mchezo huo Watford walianza vizuri, lakini hali ilibadilika pale shuti la kushtukiza la Dele Alli lilipojaa kimiani kupitia kwenye kona ya juu ya goli.

Tottenham iliongeza mengine mawili ndani ya dakika 11 ambapo Eric Dier aliunganisha krosi ya Son Heung-min na kisha baadaye Mkorea Son akatumbukiza goli la tatu.

Kipindi cha pili Watford walifanyamashambulizi machache, huku Son Heung-min akiendeleza ubabe wa Tottenham kwa kufunga goli la nne.
                             Dele Alli akiachia shuti la mpira wa kuzungusha lililozaa goli la kwanza
                                                                   Eric Dier akifunga goli la pili la Tottenham 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post