TRA YAKAMATA MALI ZA LUGUMI

Mali za mfanyabiashara maarufu nchini Said Lugumi, yakiwamo magari na majumba ya kifahari, zimeanza kushikiliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA), ikiwa ni hatua ya kushinikiza alipe malimbikizo ya kodi anayodaiwa.

Nyumba hizo ziliwekwa kufuli juzi jioni na maofisa wa TRA kwa kushirikiana na Kampuni ya Udalali ya Yono ambayo ndiyo wakala wa mamlaka hiyo ya kukusanya madeni ya kodi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela, alisema Yono imepewa kazi na TRA kukusanya madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa na Zanzibar.

Kuhusu taarifa za kushikiliwa kwa  baadhi ya mali za Kampuni ya Lugumi, Mkurugenzi huyo alithibitisha kuwa habari hizo ni za kweli ambapo wanashikilia nyumba za kifahari za mfanyabiashara huyo.

Mmeniuliza kwamba mmesikia nyumba za Lugumi zimefungiwa ni kweli, amefungiwa nyumba zake za kifahari na anadaiwa Sh bilioni 14,” alisema.
Alisema wanaodaiwa wanapaswa kulipa madeni yao TRA ndani ya siku 14 na kwamba muda huo ukipita watapewa maelekezo na serikali kama ni kuuza mali hizo ili kufidia madeni yao.
Ofisa Mwandamizi wa TRA, ambaye hakupenda jina lake litajwe alithibitisha kwamba nyumba ya Lugumi iliyoko Upanga mtaa wa Mazengo na ghorofa la kifahari lililoko Mbweni JKT, Dar es Salaam zinashikiliwa na mamlaka hiyo.

“Hakuna siri maana mkienda kwenye hizo nyumba mtakuta alama ambazo huwa Yono wanaweka kwa nyumba inayoshikiliwa, nendeni Upanga na kule Mbweni JKT mtakuta hizo nyumba tunazoshikilia,” alisema

Naye Mkurugenzi wa Elimu na Huduma ya Mlipa kodi wa TRA, Richard kayombo alithibitisha kushikiliwa kwa nyumba hizo za kifahari za Lugumi.

“Kuna operesheni zinaendelea maeneo mbalimbali nchini kuwasaka wakwepa kodi na hizo nyumba za Lugumi ni kweli tunazishikilia kwa sasa maana anadaiwa sh. bilioni 14 ambazo ni malimbikizo ya kodi pamoja na riba”alisema Kayombo
Katika operesheni ya kukusanya madeni inayoendelea TRA iliyofanyika kwa siku saba mpaka juzi, Kampuni ya Yono iliyopewa kazi hiyo ilifanikiwa kuzishikilia mali za wadaiwa mbalimbali zenye thamani ya sh. bilioni 68.1.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post