TUNDU LISSU: NIMENUSURIKA KUPIGWA NA STEVEN WASSIRA

Tanganyika Law Society (TLS) President, Tundu Lissu speaks to Mwananchi Communications Limited (MCL) editorials during his tour at the MCL premises at Tabata Relimi in Dar es Salaam yesterday. Left is Mwananchi Newspaper Content Editor, Osiah AngetileMbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alinusurika kushambuliwa na aliyekuwa Mbunge wa Bunda, Steven Wassira katika moja ya vikao vya Bunge Mjini Dodoma.
Lissu aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi kuhusu maisha yake binafsi na mambo mbalimbali ambayo amewahi kukutana nayo, ambapo alielezea pia kesi ambazo zinamkabili, maisha ya mahabusu, familia yake, burudani anazopenda pamoja na uhusiano wake na watu mbalimbali.
Mbunge huyo alisema Wassira alitaka kumpiga baada ya maneno makali aliyomtolea bungeni wakati akichangia hoja. Miongoni mwa maneno yaliyomkwaza Wassira ni baada ya Lissu kumwambia kuwa alijiunga upinzani akidhani kuna fedha na alipogundua hakuna ndipo akakimbia kurudi CCM.
“Alichukia sana. Sasa nimetoka pale naenda chooni, nikamkuta akiwa na wabunge wengine wa CCM. Aliponiona akaanza kunifuata akiniambia kuwa atanipiga, alisema Lissu
Lissu alisema kuwa alimuona Wassira akizidi kumkaribia ambapo alikuwa akielekea kwenye kona ili ampate vizuri. “Na akikasirika anakuwa mkubwa kweli, alafu mimi mdogo. Nikawa nawaangalia wale wabunge wengine wa CCM kama wataingilia kuamua, naona hakuna anayetaka kumzuia.”
Akisimulia tukio hilo Lissu alisema, Wassira alirusha ngumi ya kwanza akaikwepa, aliporusha ya pili ikamkosa huku Wassira anazidi kusogelea, akawaza kuwa akipiga hatua nyingine moja atampiga teke, wakati anaugulia maumivu yeye atakimbia. Lakini Wassira aligeuka na kuondoka zake.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post