UAMUZI WA KAMATI KUHUSU RUFAA YA SIMBA DHIDI YA KAGERA SUGAR

Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa klabu ya Simba baada ya kushinda rufaa dhidi ya Kagera Sugar waliomchezesha mchezaji aliyekuwa na kati 3 za njano.
Kamati ya Saa 72 imeshakamilisha kazi yake kwa ajili ya kuitolea maamuzi rufaa ya klabu ya Simba iliyokuwa inaihusu klabu ya Kagera Sugar baada ya kumchezesha mchezaji wake Faki Mohamed ambaye alikuwa na kadi 3 za njano wakati Simba ilipochuana na timu hiyo.
Simba News imeongea na makamu wa Rais wa Klabu ya Simba Eng. Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kuweza kuthibitisha kushinda rufaa hiyo na hivyo kuweza kuongeza pointi tatu na hivyo kuendelea kuiongoza ligi kuu ikiwa na jumla ya pointi 61.
‘Tumefurahi sana sisi kama viongozi na wanachama wote wa Simba, tumekuwa wasikivu, watulivu katika kipindi chote hichi cha kusubiri majibu ya rufaa hii, na tunashukuru kwa Kamati ya Masaa 72 kutenda haki kwenye hili na hivyo kuweza kupata pointi 3 ambazo kisheria tunapaswa kuzipata. Sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye mechi yetu ya mwisho kanda ya ziwa dhidi ya Toto African’.
Mchezaji Mohamed Faki alipata kadi za njano katika michezo ya Kagera Sugar dhidi ya Mbeya City, MajiMaji, African Lyon.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post