ULINZI WA RAIS DKT MAGUFULI ULIVYOIMARISHWA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

Rais wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo anatarajia kuzungumza na wanajumuiya wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mkoani Dodoma.
Rais Dkt Magufuli pia mbali na kuzungumza na wanajumuiya wa chuo hicho, atahudhuria pia hafla ya maadhimisho ya miaka 10 ya chuo hicho. Chuo hicho kilianza kutoa huduma kwa mara ya kwanza Septemba mwaka 2007.
Ulinzi umeimarishwa katika ukumbi wa Chimwaga ambapo ndipo shughuli hizo zinafanyikia, na pia ndipo chuo kilipoanzi, zamani ukimilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aidha, maofisa usalama wamefunga mashine za kukagulia magari katika barabara za kuingilia chuoni hapo ili kuweza kukagua mgari yote yanayoingua ikiwa ni hatua ya kuimarisha usalama.
Kadhalika, waliokuwa wakiingia katika ukumbi huo waliamriwa kuzima simu zao hadi pale watakapotoka ndani ya ukumbi huo.
Pamoja na hilo, leo Rais atakabidhiwa orodha ya watumishi kwenye vyeti feki katika mkusanyiko huo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post