UONGOZI WAELEZA SABABU YA YANGA KUACHWA NA NDEGE ALGERIA

Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa amesema kuwa walishindwa kuondoka nchini Algeria jana baada ya kuachwa na ndege waliyokuwa wamepanga kuitumia na hata walipofika uwanjani ndege nyingine zilizokuwepo zilikuwa zimejaa.
Mkwasa ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo, alisema kuwa walidhani ndege inaondoka saa tisa jioni hivyo walipotoka hotelini saa nne na kufuka uwanjani walikuta milango imefungwa na ndege imeondoka.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga waliwasili jana kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Emirates lakini kundi lililobaki Algeria lenye wachezaji 11 walikuwa watumie ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post