USALAMA WA WATOTO WA RAIS MUGABE UPO HATARINI, WAHAMISHWA NCHI

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe imearifiwa kuwa amewahamishia watoto wake wawili nchini Afrika Kusini kufuatia usalama wao kuwa mashakani.
Watoto hao wawili, Robert Jr na Bellarmine Chatunga wamehamishiwa nchini humo ambapo mmoja alitokea Dubai na mwingine Zimbabwe na sasa wanaendelea na masomo jijini Johannesburg.
Robert Jr aliondolewa kutoka Dubai kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa, huku Bellarmine akiondolewa Zimbabwe ili aweze kutilia mkazo masomo yake akiwa mbali na familia hiyo ambayo kwa siku za karibuni imekuwa na mivutano ya kisiasa ambayo ingeweza kumfanya asisome vizuri.
Sababu kubwa imeelezwa kuwa ni suala la usalama wao ambapo wangeweza kuwa walengwa na kujikuta kwenye matatizo hasa yatokanayo na siasa za nchi hiyo. Hivyo kuwaweka mbali na familia hiyo kunawasaidia wasiwe waathirika wa kisiasa kwa hali ya uongozi nchini humo si salama.
Mwaka jana, Mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe aliibua madai kuwa, wanajeshi na viongozi wengine wa chama tawala, ZANU-PF ambao wanatamani madaraka, walitaka kumuua mwanae Chatunga.
Afrika Kusini imekua ni nchi ya makazi ya raia wengi walioikimbia Zimbabwe kutokana na uongozi wa Mugabe na kuzidi kudorora kwa uchumi.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post