USOME HAPA UJUMBE WA VITISHO ALIOTUMIWA MBUNGE HUSSEIN BASHE

Mbunge wa Nzega Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohamed Bashe amesema kuwa ametumiwa ujumbe wa vitisho na watu wasiojulikana wakisema kuwa watamfanyika kitu kibaya popote pale alipo.
Bashe ambaye yupo kwenye vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ameandika leo asubuhi kupitia akaunti yake ya Tiwtter kuwa, ametumiwa ujumbe huo uliosomeka, “Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.”
Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.

Kufuatia vitisho hivyo, Mbunge Hussein Bashe amelitaka Bunge na Serikali kutofumbia macho vitendo hivi vya wananchi kutekwa na watu wasiojulikana.
Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la Haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana.


Vitisho hivi kwa mbunge huyo vimekuja ikiwa ni siku chache tu tangu mwanamuziki Roma Mkatoliki na wenzake watatu walipotekwa na watu wasiofahamika wakiwa katika studio za Tongwe Records jijini Dar es Salaam.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post