VALENCIA MCHEZAJI BORA WA MWEZI

BEKI wa kulia wa Manchester United,Antonio Valencia amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo kwa mwezi wa tatu [Machi].

Valencia,31,ambaye ni raia wa Ecuador ametwaa tuzo hiyo baada ya kujikusanyia asilimia 71 ya kura 80,000 zilizopigwa na mashabiki kupitia ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu hiyo wa @ManUtd.

Valencia atakumbukwa kwa kuonyesha kiwango bora kabisa katika michezo minne iliyopita ya Manchester Unuted kwa mwezi Machi dhidi ya FC Rostov,Bournemouth,Chelsea na kwenye mchezo dhidi ya Middlesbrough ambao alifunga bao lake la kwanza baada ya ukame wa miaka mitatu.Pia huo ulikuwa ni mchezo wake wa 200 akiwa na Manchester United.

Nafasi ya pili imeenda kwa Marcos Rojo aliyepata asilimia 23 ya kura zote huku Ashley Young akishika nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia asilimia 6 ya kura zote 80,000.

Ikumbukwe kabla ya kutwaa tuzo ya mwezi wa Machi,tayari Valencia alikuwa ameshatwaa tuzo hiyo mara mbili katika miezi ya Novemba na Januari.Hivyo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyetwaa tuzo hiyo mara nyingi zaidi msimu huu klabuni Manchester United akifuatiwa na Zlatan Ibrahimovic aliyetwaa tuzo hiyo mara mbili katika miezi ya Disemba na Februari.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post