VIDEO: MAHAKAMA KUU KENYA YAONGEZA VIKWAZO KWA TANZANIA KUPELEKA MADAKTARI

Mahakama Kuu nchini Kenya imeongeza muda wa zuio la Wizara ya Afya ya nchi hiyo kuajiri madaktari 500 kutoka Tanzania ikiwa ni lengo la kurejesha huduma za afya zilizodorora kufuatia mgomo wa madaktari.
Awali serikali ya Kenya ilikuwa imeiomba Tanzania kupeleka madaktari 500 nchini humo kufuatia mgomo wa madakatari uliodumu kwa miezi 3 na kusababisha huduma za afya kuwa mbaya katika hospitali za serikali.
Amri hiyo ya mahakama imetolewa leo ambapo kesi inayohusisha madaktari hao imeahirishwa hadi Juni 5 mwaka huu itakapotajwa tena baada ya baadhi ya pande kutowasilisha mawazo yao.
Chama cha Wahudumu wa Afya Nchini Kenya kilipinga mpango wa serikali kuajiri madaktari kutoka Tanzania huku kikishinikiza serikali kuajiri madakatari zaidi ya 1000 ambao wamo nchini humo.
Hapa chini ni video iliyorushwa na kituo cha runinga cha KTN cha nchini Kenya.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameamua madaktari wote 258 waliokuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na Serikali ya Tanzania mara moja.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, ambapo amesema Rais Magufuli amefikia uamuzi huo kutokana na utayari waliouonesha madaktari hao pamoja na wataalamu wengine 11 lakini kwa kuwa kuna pingamizi lililowekwa huko Kenya basi Serikali ya Tanzania itawaajiri wote.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post