VIDEO: STEVE NYERERE APINGANA NA AGIZO LA MAKONDA KUHUSU FILAMU ZA TANZANIA

Juma lililopita wakati wa uzinduzi wa mabweni ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisikika akikumbushia kwa lengo la kutilia mkazo agizo lake alilokuwa amelitoa la kupiga marufuku uuzwaji wa filamu za kigeni jijini Dar es Salaam.
Agizo hilo alilitoa kwa kile alichoeleza kuwa, filamu hizo zinasababisha kudumaa kwa tasnia nzima ya filamu nchi kwani zinauzwa kwa bei rahisi na hivyo watu wengi kuzikimbilia badala ya kununua filamu za Tanzania. Aidha, alisema kuwa muuzaji yeyote atakayekamatwa akiwa anauza filamu hizo, ataonyesha mkataba alioingia na wamiliki wa filamu hizo, kwamba yeye ni msambazaji halali.
Kauli hii imepokewa kwa utofauti miongoni mwa wasanii wa filamu nchini Tanzania, huku baadhi wakiamini kuwa uamuzi huo ni mzuri na ungesaidia kukuza sanaa ya uigizaji  nchini, lakini wengine wamesema kuwa kwa kufanya hivyo hakutasaidia filamu za Tanzania kuuza.
Mmoja kati ya wanaoona uamuzi huo si sahihi ni muigizaji Steve Nyerere ambaye amesema kuwa kwa kuzuia filamu za nje kuingizwa nchini au kufunga maduka ya wanaouza filamu hizo, haiwezi kuwa sababu ya kuinua filamu zetu.
“Tunaaminishwa kwamba tukifunga maduka au tukizuia filamu za nje ndio za kwetu tutauza, uongo,” alisema Steve alipokuwa akifanya mahojiano na Global Tv.
Akitolea ufafanuzi kauli hiyo, Steve alisema, tatizo la kutofanya vizuri kwa filamu za Tanzania si kwa sababu ya filamu za nje, bali ni filamu zetu kukosa ubunifu. Tumeingia kwenye biashara na kusahau ubunifu tukiamini watu watanunua tu kwa vile zipo. Hata kipindi cha nyuma ambacho filamu za Tanzania zilifanya vizuri kimataifa, Steve ameeleza kuwa filamu za nje zilikuwa zikiuzwa nchini.
“…wakati tunashindana na Nigeria, soko la filamu za nje lilikuwepo, tumetoka hapo tumeshindana na soko la filamu za India, zote hizo ni filamu kutoka nje…Watengenezaji wa filamu zetu wameshindwa kuwa wabunifu ili watu wanunue.”
Steve amewasihi wasanii wenzake, kuangalia ni wapi walipokosea ili waparekebishe badala ya kuanza kutafuta visingizio ambavyo kiukweli havitasaidia soko la filamu za Tanzania, msikilize hapa chini.JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post