VIDEO YA ALIKIBA AKIIMBA WIMBO WA RAYVANNY WAIBUA MVUTANO MKALI

3Licha ya kuwa mwanamuziki Diamond Platnumz amewahi kuweka wazi kuwa yeye na Alikiba hawana tofauti yoyote, mashabiki wa muziki wamezidi kuwapambanisha na kuwaweka katika mazingira yanayoonyesha kuwa bado hali si shwari kati yao.
Hali hii haiishii kwa mashabiki tu, kwani hata wasanii wengine wakienda kwenye mahojiano katika vituo vya redio au runinga mara nyingi utaona watangazaji  wanawauliza, kati ya ya Diamond na Alikiba unamchagua nani? Hali hii inazidi kufanya wasanii hao waonekane wana mvutano/kutokuelewana kati yao.
Siku za hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii ilikuwa ikisambazwa video ya AliKiba akiimba wimbo wa Rayvanny ambaye yuko chini ya Diamond Platnumz. Watu wengi walimpongeza Alikiba kwa kufanya hivyo kwani ilionyesha wazi kuwa hana tatizo lolote na WCB tofauti na watu wengine walivyokuwa wakidhani.
Lakini kama wanavyosema huwezi kumfurahisha kila mtu, ndivyo ilivyokuwa kwa alikuwa Alikiba, kwani baadhi ya watu walimuona kama anajipendekeza kwa WCB. Alikiba alionekana akiimba wimbo huo akiwa ndani ya gari. Alikuwa akiimba wimbo wa Kwetu ambao ndio wimbo uliomtambulisha vizuri Rayvanny katika tasnia ya muziki.
Tazama hapa chini kuona video hiyo, kisha tuandikie maoni yako yake wewe kama shabiki wa muziki.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post