VIJANA WAUZA TAMTHILIA NA FILAMU ZA NJE WAANDAMANA KUIOMBA SERIKALI KUWARUHUSU WAUZE CD HIZO.

SHARE:

Vijana ambao ni machinga wanaouza CD za Tamthilia na filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia wakionesha cd hizo juu wakati wa ...

Vijana ambao ni machinga wanaouza CD za Tamthilia na filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia wakionesha cd hizo juu wakati wa mkutano na waandishi wa habari mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)
Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Marick Omary,akizungumza na waandishi wa habari katika Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuiomba serikali kuwasaidia na kutowafungia vijana hao kuuza cd hizo kwa kuwa zinawapatia ridhiki ya kihalali tofauti na kufanya kazi zingine zisizo za kihalali.
Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Andhuhuri Mohamedy,akichangia hoja kwa waandishi wa habari katika Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuiomba serikali kuwaruhusu wafanyabiashara hao (Machinga) kuendelea na biashara hizo ambayo inawawezesha kulisha na kusaidia familia zao na kusema kama kuna maboresho ni bora serikali wakae kwa pamoja wazungumze siyo kupiga marufuku watakufa njaa.
Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Halima Bakari,akizungumza kwa majonzi kuhusu kuiomba serikali kuweka utaratibu mzuri wa kuwaruhusu wafanyabiashara hao waendelee na uuzaji wa tamthilia na filamu za nje kuendelea kuuza kwa kuwa kuna wanawake wengi wameachana na suala la kuuza miili yao (Biashara ya Ngono) ambayo siyo halali wakajiingiza kuuza cd hizo ili wapate kipato cha kihalali kwa hiyo kuwafungia ni kuwarudisha nyuma kifikra.
Baadhi ya wauzaji wa CD hizo waliokusanyika katika eneo hilo la Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
  Vijana ambao ni machinga wanaouza CD za Tamthilia na filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia wakionesha cd hizo juu wakati wa mkutano na waandishi wa habari mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wauzaji wa CD hizo waliokusanyika katika eneo hilo la Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya maduka yaliyokuwa yakiuza CD za Tamthilia na filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia yakiwa yamefungwa kama yanavyoonekana katika Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.

Imeandaliwa na mtandao wa www.elisashunda.blogspot.com/Email:elisashunda@gmail.com /0719976633 

NA ELISA SHUNDA,DAR 
 

WAFANYABIASHARA wadogo wadogo ‘Machinga’ wanaouza filamu za kigeni wameandamana wakiomba kukutana na Rais John Magufuli ili kusikilizwa juu ya kupigwa marufuku kuuza filamu hizo hapa nchini.

Marufuku hiyo ilitolewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe, siku chache baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo mara baada ya kukutana na waigizaji wa ndani ambapo walieleza malalamiko yao juu ya filamu za nje kuharibu soko la kazi zao.

Wamachinga hao waliandamana jijini Dar es Salaam jana katika soko la Kariakoo katika Mtaa wa Aggrey ambako kuna maduka wanakoenda kuchukua mikanda ya filamu za nje ‘CD’ na kusambaza mtaani huku wengine wakiweka katika vibanda kwa ajili ya kukodishia wateja wanaohitaji.

Wakizungumza na waandishi wa habari wafanyabiashara hao walisema Waziri huyo alitoa maamuzi hayo kwa kusikiliza upande mmoja ambao ni walalamikaji bila kuwapa nafasi ya kujieleza jambo ambalo wanalipinga.

Mmoja wa machinga hao Hanzuruni Mohamed alisema aliyekuwa Waziri katika Wizara hiyo Nape Nnauye alikuwa akisikiliza pande zote kabla kufanya maamuzi na kuongeza kwamba walishakaa vikao mbalimbali kwa ajili kutafuta mwafaka lakini Mwakyembe ameshindwa kufanya hivyo.

“Nape alikuwa anafanya maamuzi kwa kufuata pande zote mbili, huyu katoa siku 10 tu kufungia filamu za nje, hapa kuna vijana zaidi 1000 fikiria tutafanya kazi gani, tukiwa panya road nchi itakuwaje tunakuomba Rais uliangalie hili sisi ni vijana wako” alisema Mohamed.

Naye Halima Bakari alisema kufungwa kwa biashara hiyo kutamwathiri maisha yake kwani alikuwa akitegemea biashara ya filamu kuendesha maisha yake na kuhudumia familia yake na kusema awali alikuwa akifanya biashara ya kujiuza biashara aliyoiacha baada ya kujiingiza katika soko la filamu.

“Mwanzo nilikuwa najiuza nategemewa na mdogo wangu yatima, sasa hivi mabosi wamefunga maduka wakisema wanaogopa kufungwa kutokana na kauli ya Waziri, sasa hivi hatuna ajira nyingine mimi ni binti bila kutoa penzi sipati kazi na kauli mbiu ni Hapa kazi tu, Rais tusaidie tutaenda wapi” alisema Bakari.

Kwa uapnde wake Maliky Ally alisema wametii kuacha kuuza filamu lakini wamaomba kusikilizwa upya ili kuwe na makubaliano yatakayohusisha pande zote kwasababu hiyo ni ajira wanaoitegemea kuendesha maisha yao. 

Imeandaliwa na mtandao wa www.elisashunda.blogspot.com/Email:elisashunda@gmail.com /0719976633

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: VIJANA WAUZA TAMTHILIA NA FILAMU ZA NJE WAANDAMANA KUIOMBA SERIKALI KUWARUHUSU WAUZE CD HIZO.
VIJANA WAUZA TAMTHILIA NA FILAMU ZA NJE WAANDAMANA KUIOMBA SERIKALI KUWARUHUSU WAUZE CD HIZO.
https://1.bp.blogspot.com/-Wd88bpzlayY/WPdJ5vLr8rI/AAAAAAAAZuU/hIfiofekFYU8sey0PsitJ-XY6CgjBAZmQCLcB/s1600/1%2B%25281%2529.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-Wd88bpzlayY/WPdJ5vLr8rI/AAAAAAAAZuU/hIfiofekFYU8sey0PsitJ-XY6CgjBAZmQCLcB/s72-c/1%2B%25281%2529.JPG
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/vijana-wauza-tamthilia-na-filamu-za-nje.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/vijana-wauza-tamthilia-na-filamu-za-nje.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy