WAAMUZI MCHEZO WA YOUNG AFRICANS, MC ALGER

Mchezo wa kimataifa wa Raundi ya Pili kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na Mouloudia Club D’Alger ya Algeria unatarajiwa kufanyika leo Jumamosi Aprili 8, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ambako utachezeshwa na waaamuzi kutoka Rwanda.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Louis Hakizimana ambaye atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na Theogene Ndagijimana akiwa mshika kibendera wa mstari wa kulia na Jean Bosco Niyitegeka ambaye atakuwa mshika kibendera mstari wa kushoto.

Mchezo huo muhimu kwa Young Africans kusonga mbele kama ilivyotokea msimu uliopita kwa kuifunga Sagrada Esperanca ya Angola na kutinga hatua ya makundi, viingilio vimepangwa kuwa Sh 30,000 kwa VIP ‘A’; Sh 20,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ wakati mzungunguko itakuwa ni Sh 5,000.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post