WACHINJAJI WA NG’OMBE KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA INDIA

india
Jimbo la Gujarat lililopo magharibi mwa India limepitisha sheria inayowafanya wote wanaochinja ng’ombe kupewa adhabu ya kifungo cha maisha.
Kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha haki za wanyama kilichofanywa marekebisho, wote watakaopatikana na hatia ya kusafirisha nyama ya ng’ombe watahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.
Huko India, Wahindu huwachukulia ng’ombe kama watakatifu, na kuwaua ni kinyume cha sheria katika majimbo mengi nchini humo.
Indian monks from the International Society of Krishna Conciousness (ISKON) along with Hindu devotees worship cows as part of Govardhan Puja celebrations at ISKON temple in Siliguri on November 12, 2015.
Lakini marekebisho hayo mapya ya kifungu cha sheria ya haki za wanyama yameifanya Gujarat kuwa jimbo lenye sheria kali kuliko mengine nchini humo.
Watakaokiuka amri hiyo watatozwa faini kubwa na kutumikia kifungo jela. Kiwango cha faini kimeongezwa kutoka rupee 50,000 sawa na TZS milioni 1.7 mpaka rupee 100,000 sawa na TZS milioni 3.4
Waziri wa nchi wa Gujarat, Pradipsinh Jadeja, amewaambia waandishi wa habari kuwa ng’ombe walikuwa ni utambulisho wa utamaduni wa India na marekebisho ya kifungu hicho cha sheria yamefanywa kwa kushirikiana na wananchi.
Waziri Mkuu wa India, Vijay Rupani, amesema kwa kurudia mara nyingi kuhusu adhabu kali watakayopewa wote watakaowachinja ng’ombe.
Sheria hiyo mpya itaanza kufanya kazi mara moja itakapopitishwa na Gavana wa Jimbo hilo.
Image result for cow slaughter

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post