WASANII WA FILAMU ‘WASHAMBULIWA’ NA WANANCHI WAKIANDAMANA KUPINGA FILAMU ZA NJE YA NCHI

Wasanii wa filamu nchini jana walikuwasanyika katika Soko la Kariakoo na kuandamana wakishinikiza kusitishwa kwa uuzwaji wa filamu kutoka nje ya nchi kwa madai kuwa zinaharibu soko la filamu za ndani.
Wasanii hao wamekuwa wakidai kuwa sababu za filamu za Tanzania kutokufanya vizuri nchini kwa miaka ya hivi karibuni ni kutokana na kuingizwa kwa filamu za nje ambazo huuzwa kwa bei nafuu tofauti na filamu za ndani.
Kwa upande wa wauzaji wa filamu hizo zinazouzwa kwa wingi Kariakoo walimtaka Mkuu wa Mkoa kufikiria upya kuhusu agizo lake la kuzuia filamu hizo kwani ndizo zinazowaingizia kipato cha kuendesha maisha yao. Lakini pia walisema kuwa si kweli kwamba filamu za nje ndizo zinazoua soko la filamu za ndani, bali ubovu wa kazi za wasanii wa Tanzania ndizo zinafanya watu wasizipende.
Mbali na wauzaji wa filamu hizo, lakini pia kuna wasanii wengine ambao hawakubaliani na hatua zilizochukuliwa na wasanii wenzao kwa kuandamana.
Steve Nyerere alipohojiwa kuhusu sakata hilo alisema kuwa, kufunga maduka, au kuzuia filamu za nje kuuzwa nchini, hakutasaidia kukua kwa tasnia yetu ya filamu kwa sababu tatizo ni kwamba wasanii wa Tanzania wamekosa ubunifu.
Kwa upande wake mwanamuziki Nay wa Mitego amesema kuwa wasanii hawa wa filamu ni kama wamechanganyikiwa kutokana na uamuzi huo wa kuandamana.

Mbali na wasanii hao, wananchi ambao ndio mashabiki na wanunuzi wakubwa wa kazi za filamu, wamewashambulia wasanii wa filamu kwa kutoa yao ya moyoni kwanini hawanunui tena filamu za Tanzania na badala yake wanapendelea zaidi filamu za nje;
 kwani lazima jini awe anatokea kwenye Kona ya nyumba ?? Na akishatokea kuna ulazima wakucheka like " HAA..HAA..HAA..HAA..HAA " 😕


Tanzania na Maajabu Yake naona wasanii wa bongomovie wanatafuta Kiki Kupitia siasa na Mpira.Kwani Kuigiza mmeshindwaaa? Tutayaona mengi sana
Hivi Kusema Movies za Nje zizuiliwe hawajui kuna Internet? Hivi nani sasa hivi anaenda kununua DVD ya Movie ya Nje? Kila kitu ONLINE sasa


Bongo movie ndo mahali pekee ambapo jambazi anakuwa mstaarabu akiingia kuvamia anavua viatu @Nyamwihularay@mgaboz @salim_alkhasas 😂😂😂😂😂😂
Hapa chini ni picha za wasanii hao walipokuwa wakiandamana katika soko la Kariakoo.

C9zoZBtW0AAEehfC9zoXpBWsAA0IeIC9zoVzhXkAAOPid

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post