WASIFU WA PROF. KITILA MKUMBO ALIYETEULIWA NA RAIS DKT MAGUFULI KUWA KATIBU MKUU

SHARE:

Prof. Kitila Mkumbo ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na mwanaharakati wa masuala ya kisiasa. Alizaliwa tarehe 21 Juni 1971 kat...

Prof. Kitila Mkumbo ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na mwanaharakati wa masuala ya kisiasa. Alizaliwa tarehe 21 Juni 1971 katika Kijiji cha Mgela wilayani Iramba, Singida. (Atatimiza miaka 44 Juni mwaka huu). Prof. Kitila hakuwa na bahati ya kulelewa na wazazi, hivyo alisomeshwa kwa misaada ya ndugu na wasamaria wema.
Alisoma katika Shule ya Msingi Mgela iliyoko wilaya ya Iramba kati ya mwaka 1981-1987 kisha akajiunga Shule ya Sekondari Mwenge (Singida) na kusoma kidato cha kwanza hadi cha tano mwaka 1988-1991 na elimu ya Juu ya Sekondari akaipata pale Shule ya Sekondari Pugu kati ya mwaka 1992-1994 akijikita katika mchepuo wa PCB (Fizikia, Kemia na Bailojia).
Baada ya kuhitimu kidato cha sita alifanya kazi ya kuvua samaki katika Bwawa la Mtera huko Iringa kwa sababu ya kuwa na hali mbaya ya kiuchumi na baadaye alipata nafasi ya kwenda kujiunga na mafunzo ya polisi kwenye Chuo cha jeshi CCP Moshi kwa muda wa miezi miwili lakini alikatisha mafunzo baada ya kuchaguliwa kujiunga Chuo Kikuu.
Prof. Kitila alihitimu shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1999 akisomea Sayansi ya Elimu (hakupata daraja la kwanza kama nilivyoandika kwenye chapisho la gazeti la mwanachi – Taarifa ile nilipewa na mmoja wa walimu wake ambaye kumbe naye hakuwa na taarifa sahihi, KITILA AMENIAMBIA SAFARI YAKE YOTE YA MASOMO ALIKUWA MWANAFUNZI MWENYE UFAULU WA KAWAIDA “AN AVERAGE STUDENT”), akaanza kazi hapo hapo Chuo Kikuu kama Ofisa Utawala, aliifanya kazi hiyo kwa miaka minne (1999 – 2003) na wakati anafanya kazi aliendelea kusoma shahada ya uzamili/umahiri (M.A) akibobea katika Saikolojia, alihitimu shahada hiyo mwaka 2002.
Kitila alifanya vizuri katika shahada ya umahiri na baada ya kufundisha Chuo Kikuu kwa miaka michache alipewa udahili katika Chuo Kikuu cha Southampton kilichoko nchini Uingereza ambako alitunukiwa shahada ya uzamivu akibobea pia katika saikolojia, hii ilikuwa ni mwaka 2008.
Kati ya mwaka 2009 – 2012, Prof. Kitila amefanya kazi kama mratibu wa kamati ndogo ya ufundi ya masuala ya UKIMWI lakini pia kuanzia mwaka 2010 hadi hivi sasa ameendelea kuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCIB (Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB).
Mwaka 2010 hadi 2012 amekuwa Makamu Mwenyekiti wa UDASA (Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam) na kisha akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UDASA Oktoba 2014 na anaendelea na wadhifa huo.
Mwaka 2009 alikuwa Ofisa anayesimamia mitihani katika Shule ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, amekuwa mhariri mkuu na mhariri msaidizi wa machapisho mbalimbali yanayohusu elimu ya saikolojia, sanaa na sayansi.
Pia, amekuwa mkuu wa Idara ya Elimu ya Saikolojia na masomo ya Mtaala katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaama kuanzia mwaka 2009 – 2012, amekuwa Mhadhiri Mwandamizi kuanzia mwaka 2011 – 2014, amekuwa Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Cha Elimu cha Dar Es Salaam (DUCE) na kufanikiwa kuwa Profesa Mshiriki katika Shule ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuanzia Julai 2014.
Kitila alianza siasa kama mwanachama wa CCM, baadaye alijiunga CHADEMA kawa mshauri muhimu wa chama hicho. Naweza kuthubutu kusema, kati ya wasomi na wataalam waliotoa mchango mkubwa kiushauri, kiuhaulishaji na kimkakati na kuifanya CHADEMA iwe chama kinachojiendesha kisasa sana leo hii, mmoja wa wasomi hao ni Prof. Kitila.
Mwaka jana (2014), Prof. Kitila alifukuzwa katika chama chake cha zamani (CHADEMA) kwa tuhuma za kuandaa waraka wa mapinduzi na kukihujumu chama hicho, Kitila alitangaza kuwa angeshirikiana na wenzake kuanzisha chama kipya ambacho hivi sasa kinajukana kama ACT – Wazalendo. Na hata rafiki yake wa siku nyingi, Zitto Kabwe amekweishjiunga na chama hicho. Hata katika chama hiki kipya yeye amekuwa mshauri mkuu. Watu nilioongea nao kutoka ndani ya ACT wanasisitiza kuwa Kitila ana mchango mkubwa na unaoonekana anapokuwa katika taasisi yoyote ile.
Prof. Kitila amekwishafanya tafiti zaidi ya 18 na zimechapishwa katika majarida ya kitaaluma ya kimataifa, amekwishaandika vitabu takribani vitatu, ameoa na ana watoto watatu.
MBIO ZA UBUNGE
Prof. Kitila hakuwahi kugombea ubunge katika jimbo lolote hapa Tanzania, muda wake mwingi amejikita katika masuala ya kitaaluma na ushauri wa mikakati ya kisiasa. Japokuwa alipokuwa mwanachama hai wa CHADEMA alifanya harakati nyingi katika jimbo la Iramba, (jimbo linaloongozwa na Mwigulu Nchemba wa CCM) na amewahi kuingia kwenye misukosuko mingi na hata kufunguliwa kesi ya kisiasa kwa sababu ya harakati zake.
Mtu yeyote yule anatambua kuwa harakati zile za Kitila jimboni Iramba (ambazo sina hakika kama amezisitisha kutokana na kuhamia ACT) lazima zilikuwa na nia ya kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu au labda miaka mingine mitano ijayo. Nachoamini ni kuwa, Kitila nadhani anajiandaa kuwa mbunge miaka ya mbele na huwenda bado ndoto hizo ziko kwenye damu yake.
MBIO ZA URAIS
Prof. Kitila hajatangaza nia ya kutaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ila sehemu kubwa ya wanachama wa ACT nilioongea nao walimtaja kama mmoja wa wanachama wa ACT wenye sifa zote muhimu za kuwa Rais wa nchi ikiwa chama hicho kitaamua kuweka mgombea urais katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.
Nilipomuuliza yeye mwenyewe aliniambia kuwa ana mipango ya muda mrefu sana ya kisiasa na kwamba ataitekeleza kwa kadri alivyoipanga bila kufuata mipango na matakwa ya watoa maoni juu yake. Kwa hiyo, Prof. Kitila naye anachambuliwa kwa sababu ana sifa, vigezo na uwezo wa kuwa Rais wa nchi, hata kama yeye mwenyewe hana mipango hiyo maana hatujui nini huwatokea viongozi mbalimbali na wakaweza kubadilisha mipango yao muda wowote mbele ya safari.
NGUVU YAKE
Sifa na nguvu ya kwanza ya Prof. Kitila ni kuwa kijana na msomi mahiri. Pamoja na kuwa wasomi wengi wanapewa madaraka na wanavurunda kama vile hawakwenda shule, bado mataifa yote duniani hayakwepi wala kukimbia dhana ya kuongozwa na watu walioelimika maana kuna wasomi wengi tu ambao ni waadilifu sana katika kazi zao, mmoja wao ni Prof. Kitila. Ukiniuliza mmoja kati ya wasomi wanaojua majukumu yao na wanayasimamia sana, ntakwambia Prof. Kitila ni mmoja wao. Nguvu na sifa hii vina maana kubwa sana kwa mtu ambaye anafikiri au anafikiriwa kuwa rais wa nchi.
Lakini jambo la pili, yeye ni mwanademokrasia thabiti na anayependa demokrasia iwe katika vitendo. Msomi huyu ni mmoja wa watu wanaoamini katika kujenga hoja na wanaopenda hoja zishindanishwe na zijadiliwe kwa uwazi na kisha hoja yenye mashiko ndiyo ipitishwe na kukubaliwa na pande zote kwa sababu ina tija kwa jamii au taifa.
Ukitembelea ukurasa wake wa “Facebook” utaona watu wanaandika jambo lolote na humuoni akigombana nao, anapingwa waziwazi na wakati mwingine anatukanwa lakini anaacha uhuru wa wanaompinga na kumtukana uendelee. (Mimi binafsi nimekuwa sipendi mtu anitukane au anidhalilishe kwenye mitandao, napenda kupingwa kwa hoja na si kutukanwa, na nakumbuka kila aliyenitukana niliishia kumuondoa miongoni mwa marafiki).
Prof. Kitila yeye ameenda mbali zaidi, yuko tayari kwa hoja na yuko tayari hata kutukanwa na kudhalilishwa, mwisho wa siku kila mtu huendelea kuwa rafiki yake kwa muktadha huo. Sifa hii ni ngumu mno kuipata kwa wanasiasa wengi, uvumilivu wao una ukomo lakini kwa Kitila ni tofauti. Nchi kama yetu inahitaji watu wa namna hii kwenye uongozi wa juu.
Jambo la tatu ambalo ni nguvu na sifa ya Prof. Kitila ni kubahatika kuwa kiongozi kila alipokaa, kusoma, kufanya kazi n.k. Amebahatika kuwa kiongozi tokea akiwa mdogo, nidhamu na kuwajali wenzake viliwavuta watu waliomzunguka kumtumia yeye awe mwakilishi wao. Amekuwa “kiranja” tokea akiwa Shule ya Msingi, Sekondari na Sekondari ya Juu. Uwezo huu wa kiuongozi uliendelea hata alipokuwa Chuo Kikuu (UDSM) kwani alichaguliwa kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) kati ya mwaka 1998 – 1999.
Watu nilioongea nao kuhusu uongozi wa Kitila alipokuwa DARUSO wananiambia alikuwa na karama za kipekee. Mmoja ambaye hivi sasa ni kiongozi mkubwa CCM na aliwahi kumpinga Kitila walipokuwa Chuo Kikuu, amenieleza kuwa Kitila alikuwa na ushawishi mkubwa kila akisimama mbele ya wanafunzi, hata kama mambo yalikuwa yemeharibika sana yalitengemaa. Kitila ni mmoja wa Marais wa DARUSO waliovuka vikwazo vya kutopinduliwa, watu waliowahi kuongoza DARUSO wanajua namna ilivyo rahisi sana kulala ukiwa Rais wa wanafunzi na ukaamka ukiwa Mwanafunzi wa kawaida.
UDHAIFU WAKE
Moja ya mambo ambayo nayatizama kama udhaifu mkubwa wa Prof. Kitila ni uthubutu unaopita kiasi. Binadamu waliofanikiwa huthubutu kufanya mambo kadha wa kwadha lakini uthubutu kwa kiwango kisicholeta madhara kulingana na mahali walipo. Jambo hili halifanywi na Kitila na mara kadhaa amethubutu kufanya mambo yaliyowagutusha wenzie.
Mathalani, alipokuwa mwanachama wa CHADEMA alikiri kuhusika katika kuandaa waraka uliopewa jina maarufu la “waraka wa mapinduzi ndani ya CHADEMA”. Waraka ule ulikuwa ni moja ya mikakati ya msomi huyu kumpigia chapuo rafiki yake wa siku nyingi “Zitto Kabwe” ili ajiandae kuongoza chama hicho kupitia kwenye uchaguzi uliokuwa ukifuata. Waraka wa Kitila na wenzake ulitafsiriwa kama njama za mapinduzi ndani ya chama, usaliti na “kitu kisichofaa”.
Uthubutu huu wa Kitila ungewezekana sana kama angekuwa anafanya kazi katika vyama vikubwa mno duniani, siyo hapa Afrika Mashariki, tena nchini Tanzania. Lazima tukubali kuwa vyama vya kiafrika vimejijenga katika mifumo migumu sana kuingilika kidemokrasia na mara nyingi vina shida kwenye eneo hilo, ndiyo maana nilishtushwa na kujua kwamba Kitila amekubali kuhusika na waraka ule wakati anatambua kuwa yuko Afrika ambako demokrasia inapiganiwa kwa matakwa ya walioko madarakani kwa wakati husika.
Kwa siasa za Afrika, hata huko ACT ambako Kitila ni mwanachama leo hii, ukijaribu kuandaa waraka kama ule wa CHADEMA, nako unaweza kuonekana kama Msaliti, mfanya mapinduzi, mhaini n.k. Ndiyo maana nasisitiza kuwa uthubutu huu unaopitiliza ni tatizo kubwa sana kwake na kwa watu waliomzunguka na tamaduni zao. Hata akiwa Rais wa nchi atazungukwa na watu mbalimbali, aliowakuta na watakaomkuta, atakuwa na jukumu la kufanya mambo kwa uthubutu wa viwango vinavyokubalika ndani ya taasisi aliyomo kuliko “kuthubutu kulikovuka mipaka” ambako kunatizamwa kama uhaini kwa tamadani na demokrasia ya Afrika.
Lakini kuthubutu huku kulikopitiliza ndiko pia kumemfanya Kitila mara kadhaa atofautiane sana na menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kwenye mambo kadha wa kadha. Ubishi, na kutokukubali mambo kirahisi au kutokukubaliana na mazingira na tamaduni za mahali ulipo, ni mambo ambayo yanamgharimu sana na nayatizama kama madhaifu yatakayoendelea kutishia ustawi wake kisiasa.
NINI KINAWEZA KUMFANYA APITISHWE
Moja ya masuala yanayoweza kumfanya Prof. Kitila apitishwe na ACT kugombea urais wa Tanzania ni kwa sababu ya “umashuhuri”. Umaarufu wa Kitila umetokana na nafasi na fursa ya kuonekana mara kwa mara katika shughuli za kitaifa za CHADEMA (wakati akiwa mwanachama), pia yeye ni mmoja wa watanzania waliowahi kushiriki katika mijadala mingi ya kitaifa na ambayo imekuwa ikioneshwa moja kwa moja katika vyombo vya habari kwa hisani ya UDASA, Vyombo binafsi n.k.
Sehemu kubwa ya watanzania wanaofuatilia habari wanaweza kuwa wanamfahamu Kitila kwa namna moja au nyingine. Kwa sababu ACT ni chama kipya na kinahitaji kujikuza na kwenda juu kisiasa, nadhani kitahitaji mtu wa namna yake ambaye akipelekwa kwa wanachi, hawatauliza huyu ni nani, katokea wapi n.k.
Lakini pia, Kitila anaweza kupitishwa na ACT kugombea urais kwa sababu ya uzoefu wake wa kumudu mazingira magumu na majukumu mengi, achilia mbali uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja majukwaani. Kitila amemudu mambo mengi toka akiwa Chuo Kikuu, kwa mfano kumudu kuongoza DARUSO na kisha kupata ufaulu mzuri (Daraja la Pili) katika shahada yake siyo jambo dogo. Mimi nimekuwa kiongozi wa DARUSO na niliona ilivyokuwa kazi kupata daraja la kwanza au la pili kwa viongozi a Oganaizesheni ile. Uongozi ule ni kushughulikia matatizo ya wanafunzi kila kukicha huku vikao vya menejimenti za chuo vinazoamua masuala ya wanafunzi vikiendelea kila kona na unapaswa kuwepo kote huko.
Lakini hata baada ya kumaliza Chuo Kikuu ameendelea kuwa kiongozi wa UDASA, Mhadhiri Mwandamizi mwenye majukumu ya kufundisha mara kadhaa kwa wiki, kusimamia utafiti wa wanafunzi wanaoelekea kuhitimu shahada za kwanza, umahiri na uzamivu, Kuongoza Idara mbalimbali na hata Shule ya Elimu ya Chuo cha DUCE, kuongoza timu za kiushauri katika mipango na mikakati ya CHADEMA na baadaye ACT n.k. Mtu anayemudu majukumu mengi namna hii ndani ya ACT anaweza kuwa Prof. Kitila pekee na huwenda chama hicho kikahitaji “A Multpurpose Presidential candidate” (Mgombea Urais anayemudu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja).
NINI KINAWEZA KUMWANGUSHA KWENYE MCHUJO?
Ikiwa ACT itakuwa na mwanachama mwingine ambaye ana sifa kumshinda Prof. Kitila (si kwa maana ya elimu tu), anaweza kabisa kupewa nafasi hii ya kugombea urais na Kitila akasaidia katika masuala mengine ya mikakati. Hii ndiyo sababu pekee ambayo inaweza kuzorotesha ndoto ambayo Kitila anaotewa, kwamba ana sifa, uwezo na vigezo vya kuongoza Tanzania.
MIPANGO MINGINE IWAPO HATACHAGULIWA NA CHAMA CHAKE (PLAN B)
Mipango mitatu hivi inaweza kufuatwa na Prof. Kitila ikiwa hatapewa kazi ya kupeperusha bendera ya ACT kwenye urais mwaka huu:
Mpango wa kwanza ni kuendelea kuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu, kazi ambayo anaifanya hadi sasa kwani yeye ni mmoja wa wataalamu wachache waliobobea na wenye uwezo mkubwa katika eneo la Elimu ya Saikolojia hapa nchini.
Mpango wa pili ni kuendelea kusaidia vitengo vya upangaji mikakati ndani ya chama kipya cha ACT Wazalendo ambacho naamini kwa uchanga wake kinahitaji wapanga mikakati wazoefu ili kukifanya kisidumae na labda kufa.
Na mpango wa tatu ni kuendeleza mchango wa ukuzaji wa fikra katika jamii ya watanzania ambayo ina matatizo makubwa katika kufanya siasa za kuvumiliana na kukubali changamoto mpya. Kitila amelimudu sana eneo hili la uelimishaji na huwenda akaendelea kulipa kipaumbele.
HITIMISHO
Safari ya kisiasa ya Prof. Kitila inaweza kuathiriwa na ukuaji au uzorotaji wa CHADEMA na UKAWA. Kwa sababu Kitila ni mwanachama wa ACT na kwa kusema ukweli, ukuaji wa ACT (utakaopelekea Kitila kufanikiwa kisiasa) kwa kiasi kikubwa utategemea sana na uzorotaji wa CHADEMA, ndiyo kusema kuwa ukuaji wa CHADEMA kwa kasi yoyote ile unaweza kuathiri sana safari ya kisiasa ya ACT na Prof Kitila mwenyewe.
Kwa mfano, hata kama ikitokea Prof. Kitila akagombea urais wa Tanzania, ikiwa mgombea wa UKAWA (ambaye atalazimika kuungwa mkono na CHADEMA) atakuwa na nguvu kubwa kwa wananchi, Kitila na ACT hawatakuwa na fursa nzuri tena, labda mpaka katika uchaguzi mwingine.
Pamoja na yote hayo, namtakia kila la heri “rafiki yangu” Prof. Kitila Mkumbo katika kufikia safari yake kisiasa na kiu ya mabadiliko ya Tanzania aifikiriayo.
Uchambuzi huu umechapishwa na Gazeti la Mwananchi la Mwezi Mei 2015, Mchambuzi ni Julius Mtatiro, Adv Cert in Ling, B.A, M.A, L LB (Student): juliusmtatiro@yahoo.com, +255787536759.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WASIFU WA PROF. KITILA MKUMBO ALIYETEULIWA NA RAIS DKT MAGUFULI KUWA KATIBU MKUU
WASIFU WA PROF. KITILA MKUMBO ALIYETEULIWA NA RAIS DKT MAGUFULI KUWA KATIBU MKUU
https://1.bp.blogspot.com/-BI7quIT0-Ww/WOcopKrMaGI/AAAAAAAAZNE/ATaHccNisAEcz0cPwd1fo_hmn2JA9kNrACLcB/s1600/xIMG_0237-750x375.jpg.pagespeed.ic.lJbZWZ55-c.webp
https://1.bp.blogspot.com/-BI7quIT0-Ww/WOcopKrMaGI/AAAAAAAAZNE/ATaHccNisAEcz0cPwd1fo_hmn2JA9kNrACLcB/s72-c/xIMG_0237-750x375.jpg.pagespeed.ic.lJbZWZ55-c.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/wasifu-wa-prof-kitila-mkumbo.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/wasifu-wa-prof-kitila-mkumbo.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy