WATANZANIA WATATU WATAKAOSAFARISHWA KUJIBU MASHTAKA YA DAWA ZA KULEVYA MAREKANI

Wakili wa Serikali Edwin Kakolaki amewasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akiomba kuwasafirisha watuhumiwa watatu raia wa Tanzania kwenda nchini Marekani kujibu tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Wakili huyo kwa kushirikiana na Wakili Veronika Matikila waliwasilisha maombi hayo kwa Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha jana wakitaka Ali Hatibu Haji maarufu Shikuba na wenzake wawili wasafirishwe kwenda Marekani kujibu mashtaka yanayowakabili.
WhatsApp Image 2017-04-11 at 10.35.21 AM
Maombi hayo yaliwasilishwa chini ya sheria ya kusafirisha wahalifu na wakili waliomba yasikilizwe kwa njia ya mdomo.
Mbali na Shikuba, watuhumuwa wengine wanaotakiwa kusafirishwa kwenda Marekani ni Iddi Salehe Mafuru na Tiko Emmanuel Adam. Pia mawakilia hao waliiomba mahakama itoe kibali cha kuwahifadhi watuhumiwa hao wakisubiri kwenda nchini Marekani kujibu tuhuma zinazowakabili.
WhatsApp Image 2017-04-11 at 10.35.21 AM (2)
Mawakili wawili wa upande wa Shikuba, Majura Magafu na Hudson Ndusyepo walisema kuwa wamesikia maombi hayo ya upande wa mashtaka na kuomba mahakama iwape muda ili waweze kupitia nyaraka walizopewa kwa kitendo cha kumtoa raia nje ya nchi si kirahisi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post