WATU WATATU WAKAMATWA NA POLISI KWA KUVAMIA MKUTANO WA CUF NA BASTOLA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kushiriki katika tukio la uvamizi wa mkutano wa wanachama wa Chama cha Wananachi (CUF) uliofanyika Vinna Hotel Mabibo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alieleza kwamba, Aprili 22 mwaka huu majira ya mchana, walipokea taarifa ya kuwa kunwa watu wasiofahamika wakiwa na silaha na wamefunika nyusi zao walivamia mkutano wa CUF na kujeruhi baadhi ya watu waliokuwa mkutanoni.
Baada ya taarifa hizo amesema kuwa waliendesha msako mkali ambapo hadi sasa watu watatu wanashikiliwa na Polisi na upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani. Lakini Kamishna Sirro amewasihi  wananchi kuheshimu sheria kwa hakutokuwa na mtu au kikundi cha watu kitakachokuwa na mamlaka ya kuwajeruhi wengine kwa namna yoyote ile.
“Kama unamalalamiko pitia polisi, au mahakamani siyo kuvamia kundi la watu wengine kama wako juu ya sheria, tunafuatilia wale wote waliohusika katika kufanya shambulio hilo na mtu mmoja aliyejeruhiwa sana anataja watu walioshambulia” amesema  Kamishna Sirro.
Wakati huo huo, Kamishna Sirro amewataka wanachama wa CUF kuendelea kuwa wavumilivu wakati Polisi wakiendelea na operesheni ya kuwabaini wahusika wa tukio hilo ili waweze kuwachukulia hatua. Amesema kuwa mtu yeyote atakayefanya tukio kwa madai ya kulipiza kisasa ajue naye sheria itafuata mkondo wake.
Mapema wiki iliyopita, watu wasiojulikana wakiwa na bastola walivamia mkutano wa wanachama wa CUF ambao wanamuunga mkono, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad na kuwapiga wanachama wa CUF pamoja na waandishi wa habari ambao walikuwepo eneo hilo.
Mtu mmoja anayetuhumiwa kuhusika katika vurugu hizo alikamatwa na wananchi baada ya wenzake kumuacha na gari walilokuwa wamkuja nalo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post