WATUMIAJI WA SIMU HATARINI KUPATA UGOJWA WA AKILI

Ingawa simu za kisasa zimeleta mapinduzi makubwa ya kisayansi na kurahisisha maisha kwa kuweka mambo mengi kiganjani mwa mtumiaji, imebainika kuwa husababisha ugonjwa wa akili.
Mtaalamu wa magonjwa ya akili ambaye ni Daktari na mwandishi wa vitabu, Dk. Larry Rosen, kupitia kitabu chake cha ‘iDisorder’, alisema kuwa asilimia 70 ya watumiaji wa simu wanadalili za kuwa na ugonjwa wa akili.
Dk. Rosen alieleza kuwa asilimia hiyo ya watumiaji hujikuta wakisikia simu zao zikiita hata kama wamezizima, hali ambayo alidai kuwa ni sehemu ya ugonjwa wa akili aliouita iDisorder.
“Unaweza kusikia kama simu yaoko inaita, na ukaingiza mkono mfukoni kwa haraka ili uitoe lakini kumbe haiiiti, unajiuliza ni sauti gani hii. Huo ni ugonjwa [wa iDisorder],” alisema Dk. Rosen.
Katika hatua nyingine, gazeti la Mwananchi limemkariri daktari bingwa wa magonjwa ya akili wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kassian Nyandidi ambaye amesema kuwa watumiaji wa simu na mitandao ya kijamii wako katika hatari ya kuugua ugonjwa wa akili unaotokana na uraibu (addiction).
Dk. Nyandidi alieleza kuwa mtumiaji wa simu anayeanza kupata dalili za ugonjwa huo wa akili, huanza pale anapokuwa anafuatilia picha au taarifa fulani kwenye mitandao ya kijamii, mwisho anakuwa hawezi kuishi bila kufuatilia matukio ya aina hiyo.
Mbali na hatari ya ugonjwa wa akili, imeelezwa kuwa matumizi ya simu kwa kuandika jumbe za maandishi kwa muda mrefu (chatting) kunaweza kusababisha matatizo ya misuli ya shingo kuuma.
Itumie simu yako kwa tahadhari kubwa ili ikupe matokeo chanya zaidi na kurahisisha maisha.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post