WAZIRI MKUU MAJALIWA AUPINGA HADHARANI UTARATIBU WA PAUL MAKONDA

Serikali imesema kuwa itahakikisha inashughulikia mtandao wa wafanyabiashara wakubwa wanaojihusisha na dawa za kulevya bila ajizi, ambapo vyombo vyote vya kisheria vimeagizwa kushirikiana kwa kusimamia sheria ipasavyo.
Lakini pia serikali imeamua kuendesha vita hiyo ya dawa za kulevya kimya kimya na kuwa mtu akibainika kuwa hana hatia basi ataachiliwa huru.
Hayo yalisemwa jana Jijini Dar es salaam na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Kupambana na Dawa za Kulevya wakati wa ufunguzi wa kongamano linalohusu mmomonyoko wa maadili na athari za dawa za kulevya lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
“Sisi hatutaki umaarufu, tunataka tuone watu wanachukuliwa. Tuwapate kuanzia mzizi mpaka kwenye jani. Tukianza kushika jani, mzizi utajua jani langu limeng’oka, utapotea. Tutafuatilia mpaka kule chini,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema kuwa kila mzazi au mlezi aone aibu, uchungu na ajutie anapoona mtoto yoyote akienda kinyume na utaratibu wa kawaida wa maisha na ni vema wakatumia nafasi yao kwa kuwahimiza vijana hao waishi maisha ya nidhamu na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.
 
“Ni ukweli usiopingika kuwa mmomonyoko wa maadili ni miongoni mwa vichocheo vinavyopelekea matumizi ya dawa haramu za kulevya,  hivyo ni matarajio yangu kuwa mtaliangalia kwa kina tatizo la mmomonyoko wa maadili ambalo kwa kiasi kikubwa linatuathiri kama Taifa katika mipango ya Serikali na maendeleo ya Taifa letu,” alisema Majaliwa.
Aidha, aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga jamii yenye  kuzingatia maadili nchini na Rais, Dkt. John Magufuli amekuwa akisisitiza Watanzania wote kuzingatia maadili katika jamii kwa kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na vitendo vyote vya rushwa na ubadhirifu.
Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Siang’a aliwaomba viongozi wa dini kuunga mkono Mamlaka hiyo kwa sababu inafanya kazi kubwa ambayo inahitaji msaada wa watu wote.
Kwa upande wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Abubakary Zuberi alisema viongozi wa dini nchini wana jukumu la kukataza maovu na kuiamrisha jamii kufanya mambo mema badala ya kuiachia Serikali pekee kufanya kazi hiyo.
Z
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Nchini, Rogers Siyanga akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
Z 1
  Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Abubakary Zuberi akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majaliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
Z 2
Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017.
Z 3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post