WEMA AWANYEA WASANII WA BONGO MOVIE, ADAI ‘TUPO KWENYE WAKATI GANI NA TUPOST VITU GANI’

Malkia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu ametumia fursa ya Sakata la kutekwa kwa Roma Mkatoliki kuwachana waigizaji wa Bongo Movie ambao wanajifanya kudai haki wakati hawana umoja pale mwenzao anapopatwa na tatizo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema  kawachana waigizaji wenzake.. “This Is Scary… Ni Janga kubwa sana kwa wasanii, kwa wananchi na Kwa Taifa letu kiujumla… Kinachonishangaza ni kuona baadhi ya wasanii wa Bongo movie wamekazana kupost eti wapo kwa Mkuu wa mkoa wakiongelea WaKorea na Waphilipino.
Aliongeza, “Mlikumbuka kumuuliza Mheshimiwa alipo Roma na Moni…??? Au ndo mambo ya kila mtu anaangalia lake…. Au labda mpaka atekwe msanii wa Bongo movie pia ndo akili itatukaa sawa…??? Oh God help Us Please… Lakini pia wala sitoshangaa hata kama akitekwa msanii wa bongo movie hakuna atakaehangaika within Us zaidi ya wananchi peke yao na watu wetu wa karibu… Tumejawa sana Unafki…!!! All in All namuonea sana huruma Nancy…. Our prayers are with u mama… Inshallah mumeo atapatikana.
Tuzidi kumuomba Mungu…..🙏🏼🙏🏼🙏🏼…. Kabla sijasahau, Tuwage tuna hata fikra za kujua tupo kwenye wakati gani na tupost vitu gani….!!! Yaani mtu kapotea siku ya pili mko busy na kupost Wakorea na Waphilipino…?? aliandika msanii huyo Instagram.
Kwa mujibu wa taarifa, Jana wasanii wa Bongo Movie walikutana na RC Makonda kutoa malalamiko yao juu ya uuzwaji wa Movie za kigeni ambazo zinaingia kiholela nchini kiasi kwamba zinaua soko la Bongo Movie.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post