WEMA SEPETU NA MAFUFU WAINGIA KWENYE BIFU ZITO KISA ROMA

Nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu na Jimmy Mafufu, wameingia kwenye katika bifu kiasi cha kufikia kurushiana maneno kupitia kitandao ya kijamii.
Wema siku chache zilizopita aliandika maneno katika ukurasa wake wa Instagram kuwa kuna baadhi ya wasanii wa Bongo Movie ni wanafiki na wanaacha kuposti ishu ya kupotea kwa mwimbaji Roma badala yake wao wako bize kuposti ishu ya kukutana na Mkuu wa Mkoa ili kuongelea ishu za filamu za Wafilipino na Wakorea.
Maneno hayo yalimchoma Mafufu aliyekuwa miongoni mwa walioposti Ishu hiyo ya Wafilipino, ndipo naye akaamua kumchambua Wema katika ukurasa wake kwa maneno ya Dharau na kashfa ambao ugomvi huo ukaingiliwa na mshabiki wa Wema (Team Wema).
Hata Hivyo Mwanaspoti lilimsaka Mafufu kutaka kujua kuliko, ambapo alisema kuwa, amechukizwa na kauli ya Wema kusema kuwa katika Bongo Movie kuna wanafiki wakati, yeye ni mmoja wa wanafki hao na vilevile hataki kupangiwa cha kuposti katika akaunti zake za mitandao ya kijamii.
“Hata kama hao Team Wema wanitukane vipi, sitaacha kusema ukweli, huyo aliyewaita Bongo movie Wanafiki, yeye ndiye kinara wao asitake kuharibu jina la Bongo Movie na asiwapangie watu cha kuposti kwani nani asiyejua kuwa yeye ni mnafiki? Sitaacha kumwambia ukweli acha watu waendelee kunitusi,” alisizitiza.
Wema alipotafutwa kutaka ufafanuzi wa kuanzisha bifu hilo na wenzake, siku yake haikupokelewa licha ya kuita kwa muda mrefu.
Mwananchi
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post