YANGA WAACHWA NA NDEGE NCHINI ALGERIA

Baada ya jana kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kipigo cha jumla ya magoli  4-1 kutoka kwa MC Alger ya Algeria, Klabu ya Yanga inaonekana bado haijatulia kiakili baada ya tukio hili jingine lililowakumba leo.
Wachezaji na viongozi wa Yanga waliokuwa waondoke nchi Algeria leo kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki wameachwa na ndege baada ya kuchelewa kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene, jijini Algers.
Msafara huo uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Charles Mkwasa ulikuwa ondoke Algeria leo kurudi nchini wakipitia Istanbul.
Wachezaji hao na viongozi walioachwa na ndege watalazimika kusubiri waondoke kesho au keshokutwa.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post