YOUNG KILLER AFUNGUKA MAZUNGUMZO YAKE NA DIAMOND ‘KUFANYA KAZI’

Rapa asiye na ‘Swagga Kabisa’ zaidi ya mistari konde yenye uzani wa uzito wa juu, Young Killer Msodoki ameweka wazi kuwa kuna mpango wa kufanya kazi na Boss wa WCB, Diamond Platinumz.
Msodoki amezungumzia mpango huo baada ya Diamond kuandika kwenye Instagram mitari kadhaa anayoikubali zaidi kutoka kwenye wimbo wa ‘Sinaga Swagga’ pamoja na Remix yake, zote zikiwa ni kazi za rapa huyo toka Mwanza.
Ingawa rapa huyo alieleza kuwa hakuna mpango wa kusainiwa katika lebo ya WCB, tayari wameshafanya mazungumzo ya kuchapa kazi pamoja.
“Diamond ni msanii ambaye anamheshimu hadi msanii mdogo, kwahiyo ni jambo la kheri sana, ni watu wachache sana ambao wamebahatika kuwa hivyo,” Young Killer aliiambia Twenzetu ya 100.5 Times Fm.
“Chochote kikitokea nadhani mtaweza kufahamu, lakini kwa sasa mtupe nafasi kidogo tupambane na hali yetu. Kuingia katika lebo ya Wasafi [WCB] hapana hakuna mazungumzo hayo, kufanya kazi kupo kwa njia nyingi, kwahiyo kuhusu kufanya kazi tumeshazungumza,” alifunguka zaidi.
Killer alianza kuonekana akiwa karibu na WCB siku chache kabla hajaachia ‘Sinaga Swagga’ ambayo kwenye video yake anaonekana akiikata simu aliyopigiwa na Diamond Platinumz kabla hajaanza kuwachana wasanii aliowalenga.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post