ZIFAHAMU FAIDA ZA KUTUMA FEDHA KWENDA MITANDAO MINGINE

FAIDA ZA KUTUMA PESA MOJA KWA MOJA KWENDA MITANDAO MINGINE
Kutuma pesa #BilaMipaka kwenda mitandao mingine ina faida zifuatazo:
  1. Kuweka usawa wa ada za mitandao ya simu pale unapotuma pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine. Sasa unatumia viwango vya mtandao wako kwa ada za kutuma pesa kwenda mtandao mwingine. Mfano: Kama unatumia Airtlel Money, utatumia viwango vya makato vya Airtel Money hata ukituma pesa kwenda Tigo Pesa na EzyPesa. Kama unatumia EzyPesa, utatumia viwango vya makato vya EzyPesa hata ukituma pesa kwenda Airtel Money na Tigo Pesa. Kama unatumia Tigo Pesa, utatumia viwango vya makato vya Tigo Pesa hata ukituma pesa kwenda Airtel Money na EzyPesa.
  2. Ilikuwa unalipa gharama mara mbili unapotuma pesa kwenda mtandao mwingine: kwanza ulikuwa unakatwa ada ya pesa unayoituma, pili ilikuwa unakatwa ada ya kumwezesha uliyemtumia kupokea kiasi chote cha pesa uliyoituma. Sasa hulipii gharama za kumwezesha unayemtumia atoe pesa yote, unakatwa ada yako ya kutuma pesa tu, na unayemtumia atakatwa ada kulingana na kiasi cha pesa anachotoa katika kila muamala anaoufanya.
Faida anazopata mtu anayetumiwa pesa kutoka mitandao mingine:
  1. Njia hii haikupangii muda maalumu wa kutoa pesa uliyotumiwa na mtu anayetumia mtandao tofauti na unaotumia wewe. Hapo awali, ilikuwa ukipokea pesa kutoka mtandao tofauti ilikulazimu kuitoa ndani ya siku saba kuanzia siku uliyotumiwa. Pesa hiyo ilikuwa inarudishwa kwa aliyekutumia kama hukuitoa ndani ya kipindi hicho cha siku saba, sasa ukiamua unaweza kuiacha kwa muda wowote unaoutaka kwakuwa pesa ipo kwenye akaunti yako.
  2. Njia hii inakupa usimamizi mzuri wa pesa yako na kukupatia kumbukumbu nzuri za miamala unayoifanya. Ilikuwa ukitumiwa pesa kutoka mitandao mingine inakuja kwa njia ya SMS (ujumbe mfupi) ambayo ilikuwa ukienda nayo kwa wakala unatoa pesa hiyo na kumbukumbu ile kutokuwepo kwenye miamala ya mtandao unaotumia. Sasa kwakuwa pesa inaingia moja kwa moja kwenye akaunti yako, kumbukumbu za wewe kutumiwa pesa hiyo pamoja na matumizi yake inakuwa sehemu moja hivyo kukuwezesha kuhifadhi, kusimamia na kufatilia kumbukumbu zako za fedha kirahisi zaidi.
  3. Njia hii inakuondolea wasiwasi wa kufutika kwa SMS (ujumbe mfupi wa maneno) ambao ulikuwa unakuja kwako pale mtu wa mtandao mwingine anapokutumia pesa, ujumbe ambao ilikulazimu kuwa nao unapoenda kwa wakala kuitoa. Ilikuwa kama umeufuta ujumbe huu kwa bahati mbaya kabla ya kuitoa pesa uliyotumiwa, pesa hiyo ilikuwa inarudi kwa aliyekutumia zinapofika siku saba toka kutumwa. Sasa pesa kutoka mitandao mingine inaingia moja kwa moja kwenye akaunti yako hivyo hata ujumbe uliopokea kukujulisha kwamba umepokea pesa hiyo utapoufuta kwa bahati mbaya, pesa yako inakuwa ipo kwenye akaunti yako.
  4. Unaweza kufanya manunuzi mbalimbali ya LIPIA moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yako ukitumia pesa uliyotumiwa kutoka mitandao mingine. Hapo kabla, ili kuitumia pesa hii unayotumiwa kutoka mitandao mingine, ilikulazimu uitoe kwanza ndipo uweze kufanya matumizi unavyotaka. Sasa kwakuwa inaingia kwenye akaunti yako, unaweza kufanya manunuzi kama bili za maji, ving’amuzi, vocha za simu, LUKU au kumtumia mtu mwingine moja kwa moja kutoka kwenye simu yako ya mkononi.
  5. Sasa unaweza kutoa kiasi kidogo tu cha pesa uliyotumiwa kutoka mtandao mwingine na kuacha kiasi kinachobaki ndani ya akaunti yako kama akiba ama kumtumia mtu mwingine kama utataka. Awali ilikulazimu kutoa pesa yote kwa mkupuo mmoja ndani ya kipindi cha siku saba unapopata SMS ya kupokea pesa kutoka mtandao mwengine wa simu. Matumizi yako unayafanya kwa muda unaoutaka kwa kutoa kiasi cha pesa unachokitaka kidogo kidogo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post