ZISOME KAMPUNI 9 ZA SIMU ZILIZOPIGWA FAINI LEO NA TCRA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini zaidi ya TZS milioni 65 kampuni tisa za simu nchini kwa kosa la kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya  9,10 na 11 ya kanuni za ubora wa huduma za 2011
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amezitaja kampuni hizo kuwa Benson Informatics Limited Smart, Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania, Zanzibar Telecom Limited (Zantel), Mic Tanzania Limited, Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL) huku akizitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatoa huduma bora.
“TCRA inawakumbusha watoa huduma wote wa mawasiliano nchini kuhakikisha mnatoa huduma zinazokidhi ubora wa sauti na upakuaji wa hali ya juu (Kudownload) pamoja na kufuata sheria za huduma ya mawasiliano ya mwaka 2011”. Alisema Kilaba
Aidha Mhandisi huyo amesema wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaoshindwa kukidhi vigezo vya ubora wa huduma kama ilivyo agizwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post