ACACIA WATAKA UCHUNGUZI HURU MCHANGA WA DHAHABU

SHARE:

Na MWANDISHI WETU KAMPUNI ya Acacia imesema ripoti kuhusu mchanga wa dhahabu aliyopewa Rais John Magufuli Jumatano ya wiki hii imejaa u...

Na MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Acacia imesema ripoti kuhusu mchanga wa dhahabu aliyopewa Rais John Magufuli Jumatano ya wiki hii imejaa upotoshaji wa hali ya juu na imependekeza kufanyika kwa uchunguzi mpya ambao ni huru ili kuweza kupata ukweli.
Katika taarifa yake ya jana, Kampuni ya  Acacia, yenye makao makuu jijini London, Uingereza, imesema kwamba, imejaribu mara kadhaa kuomba nakala ya ripoti hiyo nzima pamoja na utaratibu wa kuchukua sampuli kwenye uchunguzi huo, lakini mpaka sasa haijapewa.

“Kwa kuzingatia data tulizo nazo kwa zaidi ya miaka 20 ambazo tunaweza kuzitoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, hatuwezi kukubaliana na matokeo ya Tume. Data hizi ni data ambazo zimechambuliwa na kuandaliwa na Watanzania, wataalamu pamoja na taasisi za kimataifa na zimekuja na matokeo yanayofanana.
“Data hizi huru ambazo zinaweza kuthibitika zimeonyesha kuwa dhahabu kwenye mchanga ni chini ya asilimia moja ya kumi ya kiwango ambacho kimetajwa na ripoti ya tume. Kama data za ripoti ya tume zingekuwa kweli, Bulyanhulu na Buzwagi zingekuwa ndiyo wazalishaji wakubwa wa dhahabu duniani. Kutokana na upotoshaji huu, tunaamini tathmini mpya ambayo ni huru inahitajika,” inasomeka sehema ya Acacia kwa umma.  
Zaidi ripoti hiyo inaeleza kuwa, Acacia imekuwa ikilipa mrahaba ambao ni asilimia 4 kwa mujibu wa makubaliano kati yake na Serikali pamoja na sheria za Tanzania na kuongeza kuwa, pamoja na kuwa kweli kuna baadhi ya aina nyingine za madini kama chuma, sulphur, rhodium na mengineyo kwenye mchanga, aina hizo hazina thamani kibiashara na kampuni hiyo haipati mapato yoyote kutokana nayo.
Kampuni hiyo imesisitiza kuwa, imekuwa ikilipa mrahaba kwa mujibu wa sheria kwa madini wanayoyazalisha na kusema kuwa, katazo hilo la kusafirisha mchanga kutoka migodi hiyo miwili inaifanya kampuni hiyo kupoteza zaidi ya shilingi bilioni 2.2 kila siku, huku ikisisitiza itachukua hatua zote kuhakikisha haiendelei kupata hasara.
Taarifa hiyo ya jana imekuja zikiwa zimepita siku mbili baada ya kampuni hiyo kutoa taarifa nyingine ya kukosoa ripoti ya uchunguzi wa makinikia ambayo imewasilishwa kwa Rais.
Kupitia taarifa hiyo, Acacia ilidai kuwa, haijaona nakala ya ripoti hiyo ambayo inaonyesha kuwa kiwango cha madini kilichopo kwenye makinikia yanayoshikiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam ni mara kumi zaidi ya kiwango kilichoainishwa kwenye data zilizowasilishwa awali.
Kwa msingi huo, uongozi wa Acacia ulisema kuwa unaendelea kusubiri nakala zaidi za ripoti hiyo kwa ajili ya kutolea ufafanuzi.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: ACACIA WATAKA UCHUNGUZI HURU MCHANGA WA DHAHABU
ACACIA WATAKA UCHUNGUZI HURU MCHANGA WA DHAHABU
https://1.bp.blogspot.com/-VCTvhQHpvpo/WSpOMXix_pI/AAAAAAAAb80/9WESQ51aU3kzVF0wEgxzD-YLCTk-0qLsgCLcB/s1600/acacia-mining_620x350-300x169.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-VCTvhQHpvpo/WSpOMXix_pI/AAAAAAAAb80/9WESQ51aU3kzVF0wEgxzD-YLCTk-0qLsgCLcB/s72-c/acacia-mining_620x350-300x169.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/acacia-wataka-uchunguzi-huru-mchanga-wa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/acacia-wataka-uchunguzi-huru-mchanga-wa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy