ACT WAZALENDO WASIKITISHWA NA VIFO VYA WANAFUNZI 32 ARUSHA

Chama cha ACT Wazalendo kimetuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva vilivyotokea leo asubuhi kwa ajali ya gari lilokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Lucky Vicent ya Arusha.
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia mitandao yake ya kijamii ameandika haya machache.
Huu ni Msiba wa Taifa Zima, Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi, walimu pamoja na wafanyakazi wa Shule ya awali na msingi ya Lucky Vicent ya Jijini Arusha, vifo vilivyotokana na ajali ya basi iliyotokea katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha
ACT Wazalendo tunatoa pole kwa wazazi waliopoteza watoto wao, ndugu na jamaa waliopoteza walimu na wafanyakazi wa shule hiyo, pamoja na watanzania wote kwa ujumla. Pia tunawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapate kupona kwa haraka.
Mola awalaze pema watoto na ndugu zetu wote waliopoteza maisha katika ajali hii. Msiba huu ni wa Taifa zima.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post