AFISA MIPANGO MIJI WA LINDI ATUMBULIWA KWA KUGHUSHI NYARAKA

SHARE:

Na. Hassan Mabuye & Muhammad Salim Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameamuru kusimamishwa kazi Af...

Na. Hassan Mabuye & Muhammad Salim
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameamuru kusimamishwa kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi Ndugu Castory Manase Nkuli baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na kumilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya Ardhi.
Mhe. Lukuvi aligundua hayo baada ya kuona utaratibu wa umilikishaji wa ardhi haukufuatwa  na badala yake kuonekana kuwa na mianya ya rushwa kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa kwa kampuni ya Azimio ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais.
Aidha, Afisa Mipango Miji huyo aligundulika kuwa na kosa la kughushi kwa kujifanya ni Afisa ardhi baada ya kuandika barua na kuisaini kwa niaba ya Afisa ardhi wakati yeye ni Afisa Mipango Miji ili kuimilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate ambalo pia ni kosa kisheria.
Akithibitisha makosa hayo Kaimu Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi Bi Immaculate Senje amesema kwamba utaratibu wa umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na wana kijiji.
“Kama nyie hamna uwezo wa kumfukuza kazi basi mie namsimamisha kazi kuanzia leo hafai kuwa mtumishi wa serkali” alisema Mhe. Lukuvi na kuagiza eneo hilo lirudi na kuwa mali ya serikali “ Sasa hiyo ardhi lazima irudi itakua mali ya serikali kuanzia leo” .
katika ziara hiyo, Mhe. Lukuvi ametembelea ofisi za ardhi Lindi na kufanya ukaguzi katika Masijala za ardhi na kuangalia mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi, kisha kuwaagiza watendaji wa ardhi mkoani hapo kuhakikisha wanatoa hati kwa wakati na kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa kila mmiliki wa ardhi ili kuongeza pato la serikali.
Pia alitembelea ofisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani hapo na kupokea taarifa kutoka kwa Meneja wa shirika hilo mkoani Lindi Ndugu Gibson Mwaigomole. Katika taarifa hiyo Mhe. Lukuvi amelishauri Shirika la Nyumba la Taifa kufanya uwekezaji mkoani Lindi kwa kujenga ofisi za kisasa pamoja na Nyumba zenye gharama nafuu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi akiwa pamoja na waziri Lukuvi na watendaji wa mkoa ameeleza kuwa sekta ya ardhi mkoani hapo inachangamoto nyingi lakini ofisi yake inaendelea kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuzimaliza kabisa kwa maslahi ya watu wa Lindi na Tanzania kwa ujumla.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi kuhusu tuhuma za kumilikisha ardhi kinyume cha sheria
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) wakihakiki nyaraka na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (kulia) katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi, watendaji na viongozi wa Mkoa wa Lindi wakiwa katika mkutano wakati wa ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza kuhusu utaratibu za upangaji mijina umilikishaji ardhi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi akijieleza kuhusu tuhuma zinazomkabili mbele ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua mafaili katika masijala ya ardhi mkoani Lindi ambapo alibaini mapungufu ya kutokuwa na usahihi wa uwekaji kumbukumbu za ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi wakikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi mkoani Lindi
Ndugu Gibson Mwaigomole Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Lindi.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: AFISA MIPANGO MIJI WA LINDI ATUMBULIWA KWA KUGHUSHI NYARAKA
AFISA MIPANGO MIJI WA LINDI ATUMBULIWA KWA KUGHUSHI NYARAKA
https://2.bp.blogspot.com/-DLewvnolIqE/WQr-d1LM6eI/AAAAAAAAaf0/6IZ0l_fSf2wmP_HNW7Wbg5SM1YqCQR8WgCLcB/s1600/x1-2-750x375.png.pagespeed.ic.IN5e_i5YO-.webp
https://2.bp.blogspot.com/-DLewvnolIqE/WQr-d1LM6eI/AAAAAAAAaf0/6IZ0l_fSf2wmP_HNW7Wbg5SM1YqCQR8WgCLcB/s72-c/x1-2-750x375.png.pagespeed.ic.IN5e_i5YO-.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/05/afisa-mipango-miji-wa-lindi-atumbuliwa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/05/afisa-mipango-miji-wa-lindi-atumbuliwa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy