AFRIKA KUSINI KUENDELEA KUFUNDISHA MARUBANI WA KITANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Kamisheni ya Pamoja ya Kitaifa kati ya Tanzania na Afrika Kusini, uliofanyika mapema leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Mhe. Mahiga alieleza mkakati wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini katika kuongeza maeneo ya ushirikiano hususan katika biashara na uwekezaji.
Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Maite Nkoana – Mashabane akihutubia katika mkutano huo ambao ulitanguliwa na mkutano wa siku mbili wa Makatibu wakuu. Pamoja na Mambo mengine, Mhe. Mashabane alieleza umuhimu wa kukuza uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa hayo mawili ili kuwaletea maendeleo wananchi wa mataifa yote. Pia  alitumia fursa hiyo kutoa salamu za rambirambi kwa taifa la Tanzania kwa kupatwa na msiba ambao umepunguza nguvu kazi na wataalamu wa kizazi kijacho.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akitoa utangulizi pamoja na kuratibu ratiba ya ufunguzi wa mkutano.
Sehemu ya Mawaziri wa Tanzania na viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini wakifuatilia Mkutano.
Sehemu nyingine ya Mawaziri na Viongozi wa Serikali ya Tanzania na Afrika kusini wakifuatilia Mkutano.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Afrika Kusini ambao pia walikua wenyeviti wa mkutano huo wakitoa ufafanuzi wa ratiba kwa Bi. Mindi wakati wa mkutano huo wa ngazi ya Mawaziri.
Picha ya Pamoja ya Mawaziri na Viongozi wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini.
MAH1
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga akizungumza wakati wa mkutano baina ya wawakilishi kutoka Tanzania na Afrika Kusini kuhusu majadiliano ya awali ya mikataba na makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini yanayotarajiwa kutiwa saini kesho wakati wa Ziara ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anayetarajiwa kuwasili leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Bi. Maite Nkoana – Mashabane
MAH2
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Bi. Maite Nkoana – Mashabane akizungumza wakati wa mkutano baina ya wawakilishi kutoka Tanzania na Afrika Kusini kuhusu majadiliano ya awali ya mikataba na makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini yanayotarajiwa kutiwa saini kesho wakati wa Ziara ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anayetarajiwa kuwasili leo Jijini Dar es Salaam.
MAH3
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Bi.  wakati wa mkutano baina ya wawakilishi kutoka Tanzania na Afrika Kusini kuhusu majadiliano ya awali ya mikataba na makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini yanayotarajiwa kutiwa saini kesho wakati wa Ziara ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anayetarajiwa kuwasili leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima.
MAH4
Baadhi ya Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini wakiwa katika kikao cha majadiliano ya awali kuhusu mikataba na makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini yanayotarajiwa kutiwa saini kesho wakati wa Ziara ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anayetarajiwa kuwasili leo Jijini Dar es Salaam.
MAH5
Baadhi ya Mawaziri kutoka Serikali za Tanzania na Afrika Kusini (mstari wa mbele) wakiwa katika kikao cha majadiliano ya awali kuhusu mikataba na makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini yanayotarajiwa kutiwa saini kesho wakati wa Ziara ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anayetarajiwa kuwasili leo Jijini Dar es Salaam.
MAH6
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Bi. Maite Nkoana – Mashabane akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga (wapili kulia) wakati wa mkutano baina ya wawakilishi kutoka Tanzania na Afrika Kusini kuhusu majadiliano ya awali ya mikataba na makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini yanayotarajiwa kutiwa saini kesho wakati wa Ziara ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anayetarajiwa kuwasili leo Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………
Na Husna Saidi & Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini imekubali kuendelea kuwafudisha marubani wa Tanzania ikiwa ni sehemu moja wapo ya kukuza maendeleo ya sekta ya uchukuzi na usafiri wa anga pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga ameyabainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa  ufafanuzi kuhusu majadiliano ya awali yaliyofanyika kati ya nchi hizo mbili juu ya mikataba mbalimbali inayotegemewa kusainiwa Mei 11 mwaka huu.
Balozi Mahiga alisema kuwa katika majadiliano hayo wamejadili mikataba iliyowahi kusainiwa kwa kupima utekelezaji wake pamoja na kujadili mikataba mipya iliyojikita katika sekta mbalimbali za maendeleo zikiwemo za uchukuzi, nishati, elimu pamoja na mawasiliano.
“Katika sekta ya uchukuzi tumekubaliana kuboresha barabara, usafiri wa anga pamoja na reli hasa ya TAZARA, sisi tumenunua ndege na tunaendelea kununua zingine zitakazosafiri hadi Afrika ya Kusini hivyo nchi hiyo imekubali kuendelea kuwafundisha marubani wa Tanzania kuendesha na kukarabati ndege hizo,”alisema Balozi Mahiga.
Aliongeza kuwa mikataba hiyo inayotarajiwa kusainiwa hapo kesho imelenga maeneo ambayo yatapewa kipaumbele katika ushirikiano huo yakiwemo ya uchumi, biashara na uwekezaji pia mikataba hiyo imewekewa utaratibu wa ufatiliaji na utekelezaji wake.
Akiongea kuhusu kulinda uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Bi. Maite Nkoana – Mashabane alisema kuwa ni wajibu wa kila mmoja  kutafsiri ushirikiano wa kihistoria uliopo baina yetu na kuufikisha kwa kizazi hiki na kijacho kwani kwa kusoma tu historia katika vitabu ni rahisi kwao kusahau hivyo mkutano huo utapelekea kuendeleza na kurithisha uhusiano uliopo baina ya vijana wa nchi hizo mbili.
“Tanzania na Afrika Kusini tuna historia kubwa ya kushirikiana katika harakati za kutafuta ukombozi wa nchi zetu lakini haitoshi kuwa na urafiki wa kihistoria tu bali tuwe na urafiki utakaoleta maendeleo katika nchi zetu”, alisema Bi. Maite.
Nae Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema kuwa nchi ya Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi nne zinazowekeza  nchini kwa kiasi kikubwa hivyo tayari wana mikataba mbalimbali ambayo wanaendelea kuiboresha ili kuendelea kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.
“Tumeshaongea na Waziri mwenye dhamana ya viwanda wa Afrika Kusini kwamba kuna ardhi kubwa katika eneo la Kilombero 1 na Kilombero 2 hivyo waongeze nguvu ya kuwekeza katika uzalishaji wa sukari kwenye eneo hilo,”alisema Mwijage.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post