AFYA: SABABU YA WANAWAKE KULALA MUDA MREFU ZAIDI YA WANAUME NA FAIDA ZA KULALA UTUPU

Kulala zaidi: Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Tiba cha Duke, wanawake wanahitaji muda mwingi zaidi wa kulala kuliko wanaume.
Sababu iliyoelezwa na watafiti hao ni kuwa, wanawake hutumia ubongo wao kwa wingi zaidi wakati wa mchana kuliko wanaume, hivyo kuwafanya kuhitaji muda zaidi wa kupumzika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo wanawake huhitaji muda wa dakika 20 zaidi za kupumzika kuliko wanaume, hivyo ni vyema kumuacha mke wako, dada, mama au mpenzi wako kulala kwa muda zaidi.
Kulala utupu: Mbali na kuweka akiba ya fedha ambazo ungenunulia nguo za kulalia kwa kuamua kulala utupu, lakini hii huwa ni njia rahisi ya kuamsha hisia miongoni mwa wapenzi na hivyo kuwapatia muda zaidi wa kuweza kufanya mapenzi, hali inayoweza kupelekea kuwa na uhusiano imara na wenye furaha.
Kulala utupu pia kunaweza kukufanya kutokusikia joto sana, ambalo lingeweza kukufanya usipate usingizi murua. Mbali na hilo inaweza kuwazuia bakteria kujikusanya katika maeneo ambayo hawatakiwi.
Kulala kwa ubavu wa kushoto: Kuna faida nyingi sana kulala kwa kutumia ubavu wako wa kushoto kuliko ubavu wa kulia, mgongo au kulala kwa tumbo. Kulala kwa ubavu wa kushoto husaidia mmeng’enyo wa chakula, mfumo wa hewa, na kuusaidia moyo wako kufanyakazi vizuri zaidi.
Chumba chenye ubaridi: Kulala kwenye chumba chenye hali ya ubaridi kutakusaidia kulala vizuri, kwa mujibu wa taifiti za kisayansi. Hii ni kutokana na mwili kuweza kufanya kazi zake vizuri zaid.
Mlo wa usiku: Kula chakula kizuri na kwa wakati sahihi wakati wa usiku kutakusaidia kupata usingizi mzuri zaidi. Usipende kula vyakula vizito  wakati wa usiku au kula muda mfupi kabla ya kwenda kulala, kwani utapata wakati mgumu sana kulalal vizuri.
Mazoezi: Kufanya mazoezi wakati wa jioni kabla ya kulala kutakusaidia kulala vizuri kwani mazoezi husaidia mwili kuondoa sumu mwilini.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post