AFYA YA RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE MASHAKANI APELEKWA SINGAPORE

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesafiri kwenda Singapore kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, gazeti la serikali la Herald limeripoti.
Robert Mugabe
Kiongozi huyo wa umri wa juu zaidi duniani, ambaye amekuwa akionekana dhaifu hadharani siku za karibuni, alihutubia wajumbe katika mkutano mkuu wa Baraza la uchumi Duniani Afrika Kusini wiki iliyopita.
Shirika la habari la AFP linasema alihutubu “kwa sauti hafifu huku akiwa amejibwaga kwenye kiti”.
Gazeti la Herald linasema amekwenda Singapore kwa “uchunguzi wake wa kawaida wa kimatibabu”.
Mugabe anatarajiwa kurejea nyumbani kwa wakati kuweza kuhudhuria mazishi ya jaji mkuu wa zamani Godfrey Chidya.
Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa atatekeleza majukumu ya Rais Mugabe atakapokuwa nje ya nchi hiyo.
Licha ya umri wake, chama tawala cha Zanu-PF kilimuidhinisha Mugabe kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Katika mkutano Februari, mkewe, Grace Mugabe, alisema: “Siku moja Mungu atakapoamua kwamba Mugabe afe, basi tutakuwa na maiti yake kama mgombea kwenye karatasi ya kura.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post