AINA 5 ZA WANAWAKE AMBAO WAUME ZAO HUTAFUTA MBADALA AU KUCHEPUKA

Shakhsia (personality) ya mwanamke ina nafasi kubwa ya msingi katika kuupa nguvu uhusiano wa ndoa na kuuendeleza. Hivyo, kama ambavyo silika na shakhsia mbalimbali husaidia kuendeleza uhusiano wa ndoa, pia kuna tabia na silika ambazo huufanya uhusiano wa ndoa usiwe na utulivu. Zote kali blog inakuletea aina 5 za wanawake ambao waume zao huweza kufanya maamuzi ya kutafuta wanawake mbadala au wakachepuka… lengo ni kukufanya usiingie kwenye mtego wa kuwa miongoni mwa wanawake wa aina hiyo:

1.    MWANAMKE MWENYE KUTUMIA MABAVU:

Wanaume hawapendi aina hii ya mwanamke. Kimaumbile mwanaume anapenda awe mwenye maamuzi anayeilinda na kutetea familia yake, jambo ambalo haliendani na silika ya mwanamke mwenye mabavu ambaye hawezi kubadilika na mwenye kupenda udhibiti endelevu, jambo ambalo humsukuma mwanaume kutafuta mwanamke mbadala ambaye anatamani awe chini yake.

2.    MWANAMKE AMBAYE HASHIRIKIANI NAYE KATIKA YALE ANAYOYAPENDA:

Mwanaume anapooa anaweza asifikirie kuyaacha mambo anayoyapenda, kwa sababu hapendi kuhisi kana kwamba yuko jela. Na iwapo mkewe hatoshirikiana naye katika mambo hayo, anaweza kutafuta mwanamke mwingine ambaye anamjali na kushikiana naye mambo anayoyapenda.

3.    MWANAMKE ASIYEPENDA WATOTO:

Watoto ni kitulizo cha macho na moyo wa mke na mume. Mwanamke asiyependa watoto kuna uwezekano mkubwa kwa mume kutafuta mwanamke mwingine. Hapa mwanamke ninayemkusudia ni yule asiyependa kuzaa au asiyewajali watoto.

4.    MWANAMKE ASIYEKUWA MWELEWA NA MKOSEFU WA BUSARA:

Mwanaume anampenda mwanamke mpole, mwenye soni na mwenye adabu, lakini hampendi mwanamke aliyezubaa na asiyekuwa na uelewa na mkosefu wa busara. Hata akimuoa atamchoka na kutafuta njia mbadala. Licha ya mwanaume kutompenda mwanamke mwenye mabavu lakini hapendi ahisi kuwa anaishi na mwanamke aliyezubaa na asiyekuwa na viwango vya werevu unaochangamsha mambo katika maisha yao.

5.    MWANAMKE ASIYEJALI:

Mwanaume humtafuta mwanamke ambaye atamjali yeye na watoto wake. Mwanamke anayemuenzi na kumpa nguvu katika nyakati ngumu. Hivyo, akimuoa mwanamke asiyejali, ndoa hiyo haitakuwa na mafanikio, jambo litakalomfanya atafute mwanamke wa pili atakayejaza ombwe hilo. Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume anayachukia ni kuhisi kuwa hana umuhimu wala thamani yoyote.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post