AJAX MGUU MMOJA NDANI FAINALI YA LIGI YA UROPA

Ajax imejiweka katika nafasi ya kuweza kutinga fainali ya kwanza ya Ligi ya Uropa kwa mara ya kwanza katika miaka 21, kwa kuichakaza Lyon kwa magoli 4-1 katika mchezo wa nusu fainali.

Mshambuliaji anayechezea kwa mkopo akitokea Chelsea Bertrand Traore alifunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa, kabla ya Kasper Dolberg kufunga la pili baada ya beki kujichanganya.

Amin Younes alifunga goli la tatu, lakini Mathieu Valbuena aliipatia matumaini Lyon kwa kuifungia goli moja hata hivyo baadaye Traore akafunga la nne.
                                                                  Kasper Dolberg akiifungia Ajax goli la pili 

                  Bertrand Traore akitumbukiza moja ya magoli yake mawili aliyofunga jana
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post