ALICHOSEMA ASKOFU GWAJIMA KUHUSU SAKATA LA MCHANGA WA MADINI

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemshauri Rais Dkt Magufuli kutoruhusu mchanga wa madini (makinikia) kusafirishwa kwenda nje ya nchi licha ya kuwapo kwa vitisho vya kushtakiwa.
Askofu Gwajima ameyasema hayo leo wakati akihubiri kanisani kwake ambapo amemsihi Rais azuie makinikia hayo kusafirishwa nje ya nchi hadi tutakapojenga mashine ya kuchenjulia (smelter) hapa nchini.
“Hata kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikilie hapo hapo hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe mekundu, kama hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema sijui tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe madini hakuna kwenda” alisema Gwajima.
Aidha, Askofu Gwajima amesema Tanzania ni kama tumelogwa kwani tuna kila rasilimali ya kutufanya matajiri lakini sisi bado hatujaufikia utajiri huo, huku akisema kuongoza Tanzania inabidi uwe na moyo mgumu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post