ALICHOZUNGUMZA SIMON SIRRO BAADA YA KUTEULIWA KUWA MKUU WA JESHI LA POLISI

Simon Sirro amesema kuwa anamshukuru Rais Dkt Magufuli kwa kumuamini na kumkabidhi wadhifa huo mkubwa sana katika Jeshi la Polisi ili aweze kuwatumikia Watanzania. Sirro alisema kuwa imani kubwa ambayo Rais Magufuli anayo kwake, atakahikikisha anafanya kazi ili asimuangushe.
Simon Sirro aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi kutangaza kuwa Rais Magufuli amemteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi akichukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Sirro ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam alisema Watanzania wamuombee kwani nafasi hiyo ni kubwa na kwamba mambo zaidi ataongea leo.
Amiri Jeshi Mkuu, Dkt Magufuli tayari amemuapisha Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ambapo katika orodha, yeye ni IGP wa 10 kushika nafasi hiyo.
Hafla ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post