ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA RUVUMA AFARIKI DUNIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameitumia salamu za rambirambi familia ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ndg. Said Mwambungu aliyefariki dunia leo tarehe 12 Mei, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Magufuli amesema Marehemu Saidi Mwambungu atakumbukwa kwa uchapakazi wake, busara, uongozi mahiri, na uzalendo wake kwa Taifa alipokuwa kiongozi ndani ya Serikali na katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Ndg. Said Mwambungu alikuwa ni kiongozi wa aina yake, moyo wake wa upendo ulimwezesha kufanikiwa katika kazi zake nyingi, siku zote alipigania maendeleo ya wananchi na hakushindwa kutatua jambo kwa njia ya mazungumzo, hakika tutaukumbuka na kuuenzi mchango wake” amefafanua Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli amewapa pole nyingi wanafamilia, wanachama wa CCM, na wananchi wote walioguswa na vifo hivyo na amewaombea wapumzike mahali pema peponi, Amina.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
12 Mei, 2017
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post