ARSENE WENGER KUONDOKA ARSENAL

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema hatima yake katika klabu hiyo itaamuliwa katika mkutano wa bodi ya klabu hiyo baada ya fainali ya Kombe la FA mnamo 27 Mei.
Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 67 amekuwa na akiifundisha the Gunners tangu 1996 na mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwisho wa msimu huu.
Wenger amekuwa akishutumiwa sana na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo, na wapo ambao wamemtaka ajiuzulu kwa kutumia mabango mbalimbali likiwamo lile lililorushwa na ndege.
“Kuna mambo mengi ambayo yatajadiliwa katika mkutano wa bodi. Moja, ni nini kitamtendekea meneja,”amesema.
“Bila shaka nitaendelea kubakia. Kwa sasa tunapaswa kushughulika na yaliyopo na ni kwamba tunacheza Jumapili na tuna fainali ya Kombe la FA.”
Klabu hiyo ya London kaskazini itakutana na mabingwa wa ligi Chelsea uwanjani Wembley, tumaini pekee la Arsenal kushinda kikombe msimu huu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post